Nimepoteza kadi ya NHIF nifanyaje?

BAD GUY

Member
Jan 21, 2023
16
14
Habari zenu wana- Jamii Forums. Poleni na majukumu ya kila siku.

Naombeni msaada, nimepoteza kadi ya bima ya afya NHIF. Kwa anaejua taratibu zipoje za kupata kadi mpya, je kuna malipo yoyote yanaitajika (gharama shng ngapi)?

Pia, ofisi za NHIF kwa mkoa wa Dar es Salaam ziko wapi au wakala wa NHIF kwa manispaa ya Ilala watakuwa maeneo gani.

Nawasilisha
 
Nenda Nhif ofisi zai za kurasini au kibaha njuweni hotel pale,watakupa utaratibu.
Ila unatakiwa uwe na loss report,passport size,namba yako ya nida na 20k ya kulipia
 
Pole kaka, hiyo kadi ni muhimu mno, nenda pale KURASINII ,eneo lai BENDERA TATU , shuka kona Bandari elekea bandyarini geti no 3 .

Ukifika maeneo hayo ulizia ofisi za NHIF , hakikisha umebeba picha 3 passport size zikiwa na rangi ya blue nyuma. Uwe na tsh 20,000/= .

Pia uwe na police loss report (hii waweza ipata palepale) kwenye stationary yao. Kwa gharama ya tsh 3500/=
 
Back
Top Bottom