Nimepokonywa mapenzi. Inaumaaaa

Nimepokonywa mapenzi. Inaumaaaa

Ukisikia watu wanasema kama kusoma hujui hata picha itakufunza. Leo picha imenifunza imeniuma utadhani kanioa. Huyu mwanume nilidhani Tunapendana sana binafsi nmpenda kanipa nini? Hata sijui nampenda tu takribani miaka minne sasa tuko mbali bado tuko kwenye mchakato wa kuwa pamoja.

Well tunajua mwnaume kuishi mda mrefu bila mwanamke ni uongo ila hta kama una iba huwezi kumuonyesha mkeo au mpenzi wako mwanamke wako wa nje,labda kama umemchoka.
Hivi karibuni mpenzi wangu huyu ninaempenda sana aliniambia simu yake imeharibika so hana smartphone anatumia local call okey mi nakaona sawa tu akipata pesa atanunua sikuwa na shaka mpaka siku moja nampigia hiyo local call simu inapokelewa na mwanamke nikashtuka, nkasema labda ndugu yake nkaona nichunguze zaidi nikampigia tena dem kapokea
ananiambia jamaa kaacha simu yake hapa anachaj sasa nkajiuliza kama anachaj ww unapokea simu kama nani na msg unajibu.

Akaniuliza kwani wewe nani mbona nna maswali sana. Nikamwambia mm ni mpenzi wake , nilichojibuwa niliishiwa nguvu nakukuu
" pole wee mi ni mke mwenzio"
Nilijikuta nafreeze nikimuuliza mpenzi wangu ananiambia huyu dada ni best friend wake walibadilishana simu yaani yeye akachukua smartphone na dem anatumia yake.
Sasa nkabaki nawaza kama mlibadilishana simu kwanini umpe na namba yako na msg zako anakujibia tena kwa jeuri.

Chakushangaza mpenzi wangu ananiambia nisimuamini huyu dada anataka kuharibu mahusiano yetu. Na bado nampenda.

Wanawake wenzangu hapa inakuaje ? Je wewe ikikukuta hii utafanyaje?
Kwanza sii kweli kuwa kila mwanaume huwa anachepuka pindi awapo mbali na mpenzi/mke wake kwa sababu wapo ambao hawafanyi hivyo. N pia km unampenda mpenz wako bhac yakubid umvumilie tuu
 
Asaante ila inauma kweli nimetoka nae mbali nimeshare nae mambo yangu binafsi mengi sana nilimuamini sana. Mda mwingine najiuliza pengine alikua anatafuta njia ya kuachana na mimi akaona mi king'ang'anizi. Akaamua kunionyesha kabisa kwamba bwana ee ondoka nna mwanamke tayari.
Hapa nawaza sijui nikamate mzungu tu huku niliko duh

Mambo mengi mmeshea ya maneno au mali mumeandikisha pamoja?
Huna pawa juu yake wewe sio mke wake.. vizuri umejijua ulikuwa ndio king'ang'anizi.. sasa umejifunza itakusaidia baadae.

Hata wazungu nao ni binadamu.. yanaweza kukukumba tena zaidi ya hayo.. Inaelekea unahitaji kujitambua na kujiongeza.. badilika usiwe ulivyojiona umekuwa kwake.. ili mbeleni ufaidi..

Kila la kheri
 
Pole saaana dada.

It seeem u mvumilivu na una mapenzi ya dhati.
Can we talk
 
Hivi nani aliktupa moyo wa kupenda kipumbavu namna hii?

Hii lililo moyoni litanipasua.
 
Haya mambo haya, kuna siku nilikuwa sehemu jamaa mmoja alikuwa na dada yake wanakula kitimoto akapigiwa simu na demu wake lakini ikaonyesha hampendi huyo demu. Alichofanya alimwelekeza dada yake apokee hiyo simu ajifanye ni mchumba ake, dada mtu akafanya hivyo akamfokea dada wa watu asimfatilie tena mchumba ake mpiga simu akaomba samahani tu.
 
Hiyo ni kawaida tu sister, fuata anachokuambia jamaa,wanaume sometimes tunapitiwa
 
Pole mpendwa kama vipi we jipange tu kivingine wala usiumize sana moyo wako.
 
pole dada. badilisha title mtu mzima haibiwa wala kupokonywa anaenda kwa utashi wake. je mna mtoto au chochote cha kuwafunganisha kama mali kama sio basi uhusiano unaishia hapo unaendelea na maisha yako. all the best
 
Chakushangaza mpenzi wangu ananiambia nisimuamini huyu dada anataka kuharibu mahusiano yetu. Na bado nampenda.

Wanawake wenzangu hapa inakuaje ? Je wewe ikikukuta hii utafanyaje?

He be cheatn' on u for a long time!
Msamehe, ila mpige biti
 
Kwanza katafute tafiti jogoo mmoja anauwezo wa kuhudumia matetea wangapi halafu uje sasa nikushauri
 
Ukisikia watu wanasema kama kusoma hujui hata picha itakufunza. Leo picha imenifunza imeniuma utadhani kanioa. Huyu mwanume nilidhani Tunapendana sana binafsi nmpenda kanipa nini? Hata sijui nampenda tu takribani miaka minne sasa tuko mbali bado tuko kwenye mchakato wa kuwa pamoja.

Well tunajua mwnaume kuishi mda mrefu bila mwanamke ni uongo ila hta kama una iba huwezi kumuonyesha mkeo au mpenzi wako mwanamke wako wa nje,labda kama umemchoka.
Hivi karibuni mpenzi wangu huyu ninaempenda sana aliniambia simu yake imeharibika so hana smartphone anatumia local call okey mi nakaona sawa tu akipata pesa atanunua sikuwa na shaka mpaka siku moja nampigia hiyo local call simu inapokelewa na mwanamke nikashtuka, nkasema labda ndugu yake nkaona nichunguze zaidi nikampigia tena dem kapokea
ananiambia jamaa kaacha simu yake hapa anachaj sasa nkajiuliza kama anachaj ww unapokea simu kama nani na msg unajibu.

Akaniuliza kwani wewe nani mbona nna maswali sana. Nikamwambia mm ni mpenzi wake , nilichojibuwa niliishiwa nguvu nakukuu
" pole wee mi ni mke mwenzio"
Nilijikuta nafreeze nikimuuliza mpenzi wangu ananiambia huyu dada ni best friend wake walibadilishana simu yaani yeye akachukua smartphone na dem anatumia yake.
Sasa nkabaki nawaza kama mlibadilishana simu kwanini umpe na namba yako na msg zako anakujibia tena kwa jeuri.

Chakushangaza mpenzi wangu ananiambia nisimuamini huyu dada anataka kuharibu mahusiano yetu. Na bado nampenda.

Wanawake wenzangu hapa inakuaje ? Je wewe ikikukuta hii utafanyaje?
Me nilipitia situation kama yako hii uyo kaka anaishi na uyo mwanamke asikupoze kwa maneno ya kusema usimwamini jua tu kua anaishi nae uyo Dada pole sana jiandae kisaikolojia rafkangu japo ni ngumu coz unampenda mshikaji apo utashangaa kashampa na mimba tyari....jiandae tu me yalinikuta kama ya kwako nilikubali kuachia ngazi na kumove on japo ilikua ngumu but nw am fine
 
Back
Top Bottom