Nimepokonywa mapenzi. Inaumaaaa

Nimepokonywa mapenzi. Inaumaaaa

Fifi J

Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
47
Reaction score
48
Ukisikia watu wanasema kama kusoma hujui hata picha itakufunza. Leo picha imenifunza imeniuma utadhani kanioa. Huyu mwanume nilidhani Tunapendana sana binafsi nmpenda kanipa nini? Hata sijui nampenda tu takribani miaka minne sasa tuko mbali bado tuko kwenye mchakato wa kuwa pamoja.

Well tunajua mwnaume kuishi mda mrefu bila mwanamke ni uongo ila hta kama una iba huwezi kumuonyesha mkeo au mpenzi wako mwanamke wako wa nje,labda kama umemchoka.
Hivi karibuni mpenzi wangu huyu ninaempenda sana aliniambia simu yake imeharibika so hana smartphone anatumia local call okey mi nakaona sawa tu akipata pesa atanunua sikuwa na shaka mpaka siku moja nampigia hiyo local call simu inapokelewa na mwanamke nikashtuka, nkasema labda ndugu yake nkaona nichunguze zaidi nikampigia tena dem kapokea
ananiambia jamaa kaacha simu yake hapa anachaj sasa nkajiuliza kama anachaj ww unapokea simu kama nani na msg unajibu.

Akaniuliza kwani wewe nani mbona nna maswali sana. Nikamwambia mm ni mpenzi wake , nilichojibuwa niliishiwa nguvu nakukuu
" pole wee mi ni mke mwenzio"
Nilijikuta nafreeze nikimuuliza mpenzi wangu ananiambia huyu dada ni best friend wake walibadilishana simu yaani yeye akachukua smartphone na dem anatumia yake.
Sasa nkabaki nawaza kama mlibadilishana simu kwanini umpe na namba yako na msg zako anakujibia tena kwa jeuri.

Chakushangaza mpenzi wangu ananiambia nisimuamini huyu dada anataka kuharibu mahusiano yetu. Na bado nampenda.

Wanawake wenzangu hapa inakuaje ? Je wewe ikikukuta hii utafanyaje?
 
Mkuu usijal hpo unaanza kukomaa na maumivu ya mapenzi, inatakiwa upitie maumivu tena kama mara 3 hivi, baada ya hapo unakua concord hutokuja umia tena. Mapenzi yapo yasikutawale, ila uyatawale. Na uyachukulie ni kitu cha kawaida sana (najua sasa hivi itakua ngumu kunielewa ila tutaelewana kidogo kidogo ngoja tuoneshane makali ( in dk shika )) ...

NOTE: tambua unapendwa na watu wengine wazuri tu kuliko huyo ngurumbili anayekutesa, sasa uking'ang'ania utakua kipofu hautaweza kuona hao wanaokupenda.

Mwisho, pole sana ila ndio vzr unazidi kukomaa kiakili na kimapenzi, na ninapenda ikutokee tena ili uyazoee.
 
Pole

Usipokee simu zake tena.. Smartphone amekuwa anatumia kama kawaida. Inakuwaje hujaenda alipo!! Ila mshukuru Mola umemjua mapema.. fikiria mwingine amekuwa anakutaka labda atakusaidia kampani ya maongezi kwa sasa..

Anakujibu hivyo ili asikuumize kilichobaki ni kuamua wewe.

Halafu hujapokonywa.. yeye ndio ametaka iwe hivyo.
 
Pole

Usipokee simu zake tena.. Smartphone amekuwa anatumia kama kawaida. Inakuwaje hujaenda alipo!! Ila mshukuru Mola umemjua mapema.. fikiria mwingine amekuwa anakutaka labda atakusaidia kampani ya maongezi kwa sasa..

Anakujibu hivyo ili asikuumize kilichobaki ni kuamua wewe.

Halafu hujapokonywa.. yeye ndio ametaka iwe hivyo.
Asaante ila inauma kweli nimetoka nae mbali nimeshare nae mambo yangu binafsi mengi sana nilimuamini sana. Mda mwingine najiuliza pengine alikua anatafuta njia ya kuachana na mimi akaona mi king'ang'anizi. Akaamua kunionyesha kabisa kwamba bwana ee ondoka nna mwanamke tayari.
Hapa nawaza sijui nikamate mzungu tu huku niliko duh
 
Back
Top Bottom