Nimepiga chabo sana semester nzima kuelekea UE msaada tafadhari

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,304
25,033
Jamani eeh ,,,nimepiga chabo semester nzima na nimehudhuria vipindi vichache sana na kusoma kwangu naona uvivu sana

Pepa zote nimefaulu kwa chabo kwa kuigilizia kwa wenzangu au kuingia na simu kwenye pepa ,,nikiona sipo comfortable zaidi naomba ruksa naenda kugoogle maswali chooni au kuangalia majibu kwenye slides za kwenye simu

Sasa jamani UE inakaribia halafu kupiga chabo ni vigumu kwa sababu wasimamizi wanakuwa wengi na msimamizi akikudaka unapiga chabo halafu akakupeleka ngazi ya juu anapewa laki 2 yake ,,,,,sasa hapa nilipo nawaza kila ninachokisoma sikielewi kwa sababu nimedoji vipindi vingi na mitihani ndo kama hivyo inakaribia

Je nifanye nini ili nifaulu???
 
Wasomi wa mwendokasi hawa. Ingekuwa enzi zetu solution ilikuwa rahisi na ya uhakika ..... unaomba kurudia mwaka. Hii ilikuwa inatusaisia ili kumaster masomo yako, sio kupata alama za juu tu ambapo mbeleni hazina faida yeyote
 
Mzazi unamuingiaje mpaka akuelewe urudie mwaka.
 
Jamani eeh ,,,nimepiga chabo semester nzima na nimehudhuria vipindi vichache sana na kusoma kwangu naona uvivu sana

Pepa zote nimefaulu kwa chabo kwa kuigilizia kwa wenzangu au kuingia na simu kwenye pepa ,,nikiona sipo comfortable zaidi naomba ruksa naenda kugoogle maswali chooni au kuangalia majibu kwenye slides za kwenye simu

Sasa jamani UE inakaribia halafu kupiga chabo ni vigumu kwa sababu wasimamizi wanakuwa wengi na msimamizi akikudaka unapiga chabo halafu akakupeleka ngazi ya juu anapewa laki 2 yake ,,,,,sasa hapa nilipo nawaza kila ninachokisoma sikielewi kwa sababu nimedoji vipindi vingi na mitihani ndo kama hivyo inakaribia

Je nifanye nini ili nifaulu???
Okay....upo chuo sio? Hongera, UE yako ya ngapi hii?
 
Sielewi sasa ,,topics zimeanza mpaka zimeisha sijawahi kuhudhuria

Kila nachosoma naona maluweluwe tu.
Kuwa serious huna tofauti na mm enzi za chuo nilikuwaga na doji sana but pepa likikalibia natafuta chimbo na soma mwanzo mwisho hata kama topic siielewi nitajilazimisha hivyo hivyo na ninatafuta msaada kwa marafiki wanielekeze lakin kuingia na kizenga au kupiga chabo kwangu ilikuwa nooooooo. Mwisho wa siku nilifaulu vzr na kuhitimu vyema nakushauri achana na chabo wala sijui simu ukikamatwa huna chuo....pangilia mambo yako vzr weka kichwa chako vyema soma hata kama ni kwa zima moto at the end utafaulu vzr tu
 
Mzazi unamuingiaje mpaka akuelewe urudie mwaka.
Vitu kama hivi hutakiwe kumshirikisha mzazi. yeye atakuja kufahamu baada ya maamuzi kufanyika na kutekelezwa. hapo hata akiuliza kulikoni unampa laivu wala hatakuwa na cha kusema
 
Back
Top Bottom