Ndugu cha kwanza cha kuelewa.
Huwezi kufanya kila biashara, hata kama mtaji unao, yaani inahitaji mtaji wa Millioni 20.
Kukupa ushauri inahitaji mambo kadhaa. Ingawa hujasema mengi , nitashauri kufuatana na machache uliyosema.
1. Umepewa 20 MLN. kwamba huu si mkopo toka benki na hauna riba. Pengine ni mkopo tu utarudisha hela kamili baada ya kipindi fulani.
2. Wewe binafsi una uzoefu kwenye biashara gani? Je umewahi kuajiriwa katika eneo fulani na hivyo unajua mzunguko wa biashara hiyo hivyo kwa kuangalia uzoefu wako unaweza unaanzisha kitu fulani.
3. Angalia biashara zilizopo na uchunguze kwa makini ni eneo gani unaweza kuingia , ukafanya biashara kwa njia tofauti , au ukatibu tatizo fulani lililoko kwenye eneo hilo kwa kufanya biashara .
4. Lenga kufanya biashara ambayo unaweza ukaanza kidogo na halafu ikawa na uwezo wa kupanuka na isihitaji usimamizi wako kwa karibu. Biashara ambazo inaweza kuwa na automation system au checking system, ambazo ukienda unaweza ukacheki vizuri.
5. Unaweza kuanzisha biashara ambayo kama wewe huna uzoefu , basi unaweza ukawapata wazoefu ukawaajiri na hapo hapo ukiendelea kujifunza pole pole.
6. Anzisha biashara kufuatana na haiba yako. Ukijiangalia mwenyewe , je unaweza kukidhi vigezo vya kufanya biashara katika eneo husika. Mfano, unataka kuanzisha biashara ya udalali wa matunda na mboga mboga - Sokoni Kariakoo. Hapa unahitajika kuamka mapema karibu saa tisa ya usiku kila siku. Je unaweza kuamka muda huo kila mara.
Baada ya kusema hayo wewe mwenyewe utajipima na kuangalia ni eneo gani moyo wako upo tayari kufanya na kuendelea kukuza biashara yako.
Angalia biashara zilizopo na uamue kufanya kitu kipya na umaanishe unaweza kufanya biashara.
Kwa msaada wa mawazo . Aanzisha biashara za huduma, lakini zinazolenga kutoa bidhaa halisi.
Mfano. Unaweza kuanzisha fast food ya gharama ndogo - Unahitaji majiko ya kisasa na mandhari nzuri na uwe karibu na barabara ambapo wateja wanaweza kufika kwa urahisi. Halafu tizama majirani wanaokuzunguka, kama kuna taasisi zozote , shule binafsi, lenga kuwapelekea chakula maofisi . Ukianzia vitafunwa, chakula cha mchana . Hapa utakuwa na masoko mawili, wale wanaokuja kula pale kwenye mgahawa na wale utakaokuwa unapelekea outside catering .
Kufanya outside catering, huitaji hela nyingi. Kuna bodaboda kibao , unampa tenda au unanunua ya kwako unafanya delivery kwa urahisi kabisa.