Nimepewa million 20 mkononi, niifanyie nini?

Nimepewa million 20 mkononi, niifanyie nini?

Jenga nyumba alafu ipangishae.. Real estate ndio biashara ya mjini hapa
 
Huyu jamaa hana hizo 20m. Labda ungeandika kama nikipewa 20m mkononi nifanyie nini. Ninaandika hivi sio kwa sababu nina chuki la hasha. Kwa logic ndogo tu ni kuwa huwezi pewa 20m bila sababu. Nashauri atoe maelezo ya kutosha ili tumshauri kikamilifu.
 
Njoo nikuuzie kiwanja ambacho nawe utaweza kuja kukiuza baaadae kwa bei ya juu zaidi kama huna cha kufanyia kwa sasa. Ni PM
 
Kanunue madawa ya kulevya iishe ( au nenda kwa business developers)
 
huo ndio ubaya wa pesa kuanzia mkononi badala ya kichwani. ili uweze kushika na kuendeleza pesa ni lazima pesa ianze kuonekana kichwani. unapanga na kujiridhisha mfano nitanunua mbuzi mtera iringa kwa 40,000@ nitawafikisha pugu kwa gharama ya 5000@ nitawauza kwa 60.000 mpaka 70,000@ nakuibuka na faida ya 10,000 mpaka 20,000@.
kama kweli umepata hiyo 20ml kainunulie vipande vya mfuko wa uwekezaji au kuna watu na mashirika meeeengi wanakopesha pesa kwa wafanyabiashara kwa riba ya 20%, 30% 50%, 60% per month. kuna ndugu zangu na marafiki zangu wana biashara hizi.. kubaliana uwekeze kwenye mfuko mtagawana kadri mtakavyokubaliana. kuna soko la fedha linazidiwa uhitaji(demand ni kuubwa saana kuliko supply). wakati huo uwe unajitathmini unapenda uweje katika maisha yako; kuwa mfanya biashara au mwekezaji?
 
Back
Top Bottom