Nimependwa na askari jeshi wa kike!

Muoe tu! Ila kabla hujaoa njoo hapa karume ununue mabuti ya uhakika.Then jenga kachumba kadogo ka emergence ili kikinuka ukalale humo.Mwisho kabisa usikubali eti akutoe out.Dah hapo lazima atakupeleka lugalo
 
Umenikumbusha JKT harakati za maafande na akina dada wa mujibu wa sheria. Najua hii vijana wa kisasa hawawezi elewa nazungumzia nini.
 
Ufanyeje kivipi????

Moyo wako unasemaje juu yake???

Usihofu kazi yake wewe unaoa mtu sio kazi yake

Shida yako ipo wapi mbona sioni?????
 
dah...me napenda sana mademu wajeda au polisi tena wakiwa weupe!! weeee kama yupo humu mmoja ani PM
 
tatizo ni haya maneno ya mtaani.

Lisemwalo lipo MITISHAMBA, japo maneno ni maneno tu, hata kwenye kanga yapo, lakini siyo kuyapuuza. MImi kwa ushauri wangu, kama upo tayari kusema "NDIYO AFANDE" muoea. lakini kama haupo tayari, tafuta MCHINA mmoja, akufundishe Karate kidogo, siku hizi wengi sana mtaani, hadi machinga. vinginevyo, ndoa inaweza kuwa ndoano.
 
niliwahi sikia kuwa kwa wanawake kwa mujib wa maadili ya kaz yao ndo yatakiwa iwe ni kwa wajeda wenzao sina hakika kwa hili lakin pia waweza lifanyia utafiti,lakin wanajamvi hivi ndoa c makubaliano baina ya wapendanao mi nadhan amchunguze vizur akiona inampendeza co mbaya ila ajiridhishe kwanza na muhusika kwa kumfuatilia mtuwe akilinganisha na kuyapembua mawazo ya wanajamvi
 
Umenikumbusha JKT harakati za maafande na akina dada wa mujibu wa sheria. Najua hii vijana wa kisasa hawawezi elewa nazungumzia nini.

fafanua zaidi sasa ili watoto wadogo waelewe tunachokielewa watu wazima
 
Back
Top Bottom