Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,204
- 3,277
Nimependa sana utaratibu wa Kenya. Kule unaishi kwa jasho lako, hali ya soko au demand inaachwa iongee yenyewe, hakuna chombo cha kupanga bei ya Nauli ya bus au daladala. Kule nauli inabadilika kadri ya mahitaji ya wakati huo, mfano asubuhi unaweza kupanda daladala kwenda kilomita 15 kwa Tsh 1500, lakini mchana urefu huo huo ukasafiri kwa Tsh 500.
Mimi nimependa sana namna hii ya uchumi, kwamba inawafanya watu wafanye kazi kwa bidii bila kusubiri serikali kuwatetea kwa kupenda "cheap life". Haiwezekani mtu kajituma, kanunua Hiace yake, halafu umpangie nauli kuwa ni shilingi 300. Hii tabia ya serikali yetu kuingilia biashara za watu inajenga tabia ya uzembe na umwinyi. Kuna kituko kingine nimesikia eti wananchi wanataka serikali itoe bei elekezi ya nyumba za kupanga, kwa mfumo huu wa umwinyi itatuchukua muda mrefu kuwa na fikra za kujitegemea ikizingatiwa kuwa dunia siyo kisiwa. Tuache soko liongee, watoa huduma wakikosa wateja watashusha wenyewe bei, kama ambavyo Wakenya wanashusha bei wenyewe kwa kutegemea nyakati