Unajua kinachoshangaza watu ni kwamba, Je cdm wote hawakua bora kupata mgombea kwenye maisha yao yote ya kisiasa mpaka mtu alietoka upande wa wa pili aje awatetee kwenye nafasi hiyo?Kuna kundi limeibuka ghafla wakijifanya kuwa na uchungu sana na CHADEMA kumbe ni wanafiki, moyoni wako CCM. Wakati Magufuli anatangazwa kundi hilo hilo liliibuka na kuwashauri CHADEMA wakomae na ubunge. Ujio wa Lowassa umeonyesha rangi za baadhi ya watu. Sasa ni kama wamechanganyikiwa na kujifanya washauri wa CHADEMA.
Mimi nilikuwa mmoja wa watu niliyempinga Lowassa na kumuita mwizi wakati wa mchakato wa kura za maoni CCM ili asipitishwe sababu kubwa niliona upepo wake ulikumba hata wasiokuwemo. Nilijua wakimpitisha tu wapenda mageuzi tumekwisha kwani upepo wake ungepiga hadi kwenye majimbo ya upinzani, na badala ya kuongezeka yangepungua. Kuna wabunge wengi wa CCM walitegemea sana upepo wa Lowassa uwapitie. Sasa hivi wamechanganyikiwa wanaomba bora wangejitoa CCM mapema kabla kura za maoni CHADEMA hazijafanyika.
Ndugu zangu upepo wa wanasiasa ni mbaya sana kuna wabunge CHADEMA upepo wa Dr.Slaa uliwapitia hadi leo hawaamini kama wapo mjengoni. Lowassa upepo wake ni mbaya sana. Dr.Slaa angemsumbua Dr.Magufuli lakini asingemshinda. Vile vile kwenye UKAWA ujio wa Lowassa umeleta mshikamano zaidi. Ninaamini kuna wana CUF na NCCR wasingeweza kumpigia kura Dr.Slaa zaidi ya wabunge wao. Lakini Lowassa ni kama amekuja kuwaunganisha UKAWA. Zitabebwa kura nyingi sana hapa.
Hawo wasiomtaka Lowassa ni wale waliotaka wapinzani wawe wapinzani milele. Ndio wale utawaskia Urais CCM, Ubunge upinzani. Huo ni unafiki mkubwa. Tunahitaji CCM itoke kabisa. Sasa ujio wa Lowassa ni kama umewachanganya sana wamebaki kujifanya wanakishauri chama kumbe wanafki wakubwa. Lengo kuu la chama ni kushika dola kama kuna upenyo umetokea wa kukupeleka huko utumie ipasavyo. Muda ndio huu ukipita CCM itatawala milele.
Unajua kinachoshangaza watu ni kwamba, Je cdm wote hawakua bora kupata mgombea kwenye maisha yao yote ya kisiasa mpaka mtu alietoka upande wa wa pili aje awatetee kwenye nafasi hiyo?
Sasa hivi mnatumia nguvu nyingi sana kuwaaminisha watanzania eti Lowassa ni msafi lakini kamwe na hamtaeleweka, itawasumbua sana hii na mtapata shida kubwa sana
Ni vizuri mtoa mada ukajua nini lengo la UKAWA na wananchi kwa ujumla. Sisi wenye uchungu wa ukweli na nchi hii ya neema nyingi tunakushauri ujue kuwa swala siyo mtu bali ni kuweza kufanya mageuzi yenye tija kwa faida ya kila mwananchi. Lowasa anakubalika na dunia nzima. Tumpe nafasi atupe mwanzo mzuri.
Kama kuna kosa CHADEMA watalijutia ni kumfanya Lowassa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo.
Chama sasa hakina tofauti na CCM kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama.
Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono CHADEMA wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa.
Pole Dr Slaa lakini Mungu yuko na atatunusuru.
Nafasi ya mgombea urais Chadema imeuzwa kwa mtu binafsi.
Wafuasi walioamini mabadiiko ya kweli wakumbuke kuwa tuliwaonya kuwa Chadema ni Chama cha kilaghai...