NIMEPATA MTOTO WA KIUME

Hongera sana mkuu.
Kikubwa ahudhurie clinic asikilize anashauriwa nini na wataalamu.
Fuata ushauri wa mama zenu pande zote mbili hao ndiyo wanajua zaidi.
Shukran sanaa... Hlo nmewaachia mama yake mke wangu na bibi yangu mzaa baba wamwangalie vzr...
 
Shukran sana kwa ushauri mzuri wa malezi...
 
Mama asishike mimba kwa angalau zaidi ya Miaka miwili!
 
Kwakweli nipo makini snaa... Toka alvokuwa mjamzito karbu clinic zote meenda nae
Mashallah, hongereni sana

Ahudhurie clinic maa wa mtoto aweze kupata chanjo na kupimwa uzito na mengineyo ambayo mama akienda huko au mkienda pamoja mtayapata
 
Google au nenda hospitali hizi za private wanafundisha mambo hayo yote unayoyataka .
 
Duh mkuu utaua , mtoto hata mwezi hajafika unaongelea mambo ya bakora[emoji1] [emoji1]
Hahahaha hata mimi nilitaka shula essay moja matata ila nikaona nisimchoshe maanasiku mbili bado sana kumtia funzo la hawa manunda wetu waliogika minne nk
 
Mkuu wewe kam baba ukileta uanaume wa dar kwenye malezi utampoteza mtoto. Komaa kiume, mtoto alelewe kwa misingi ya kiafrika na ya kidini, ukiendekeza uzungu kwenye familia yako utampiteza mtoto..

Kuna hii kasumba ya wazazi wajinga, mtoto akifikisha miaka mitatu anapelekwa day care eti hawana muda pumbaaaafu kabisa, kama ulijua huna muda kwann ulifuni chupi yako ukapata mimba??

Angaia sana mwanao anapoenda shule za bweni... Mara kadhaa mashoga wanaibukia huko. Ila kama utampa misingi mizuri ya malezi hasa kidini jua ata savaivu!!

Narudia tena, wewe kama baba ukileta upuuzi na upumbafu wa kizungu jua kabisa mtoto huyu unamfurahia leo kuna siku utampoza kizembe!!

Yangu ni hayo.

NB: Sikupi pongezi maana kuzaa ni wajibu wako, na kwa sababu ni wajibu sioni maana ya kukupa pongezi.

Kila la heri.
 
Hongera sana mkuu. Kwanza zidisha upendo kwa mama yake, jitahidini mtoto anyonye maziwa ya mama yake tu kwa miezi sita ya mwanzo. Hakikisheni anapata chanjo zote kwani ni muhimu sana,analazwa kwenye chandarua ili kumkinga na malaria na msiruhusu abebwe hovyo na kila mtu wengine wana mafua makali watamuambukiza mtoto. Pia kama ni waislamu mfanyieni dua ya akika pindi anapotimiza siku 7.
 
Shukran sana Inshaallah...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…