Nimepata kikohozi kisichoisha naomba msaada

Nimepata kikohozi kisichoisha naomba msaada

machiaveli

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
2,336
Reaction score
5,323
Habari zenu wakuu?

Nina tatizo la kukohoa kwa muda mrefu nilienda hospital wakanipima makohozi kuangalia kama Nina tb lakini sikuwa nayo wakanipiga xray ya kifua wakaniandikia dawa za pneumonia nikapata nafuu kidogo lakini hali ikajirudia ile ile!

Nikarudi tena wakaniandikia tena dawa za minyoo lakini haikusaidia,kikohozi ni kikavu muda mwingi na hasa nikipigwa na ubaridi nyakati za usiku!

Kinanyima raha sana kimekua kero kwangu na kwa watu,msaada tafadhali hili ni tatizo gani na ni wapi naweza kupata tiba? Sivuti sigara wala bangi
 
Huwa wakohoa zaidi mchana au hata usiku pia (ukiwa umelala usiku wapata pia kikohoo)?
 
Kuna uwezekano mkubwa ukawa na mzio ktk njia yako ya hewa.

Je, kifua huwa hakibani?
 
Huwa wakohoa zaidi mchana au hata usiku pia (ukiwa umelala usiku wapata pia kikohoo)?
Jibu swali hilo halafu ntachangia kitu maana nliwahi pata tatizo hilo kipindi fulani hivi nikapata dawa
 
Habari zenu wakuu?
Nina tatizo la kukohoa kwa muda mrefu nilienda hospital wakanipima makohozi kuangalia kama Nina tb lakini sikuwa nayo wakanipiga xray ya kifua wakaniandikia dawa za pneumonia nikapata nafuu kidogo lakini hali ikajirudia ile ile...
Mdogo wangu pia alihangaika na tatizo hili, siku moja tukajaribu kumtafutia dawa ya asili(miti shamba),tangu amalize hiyo dawa hakuumwa tena ni miaka kama 15 imepita hasumbuliwi kabisa na hilo tatizo
 
Mdogo wangu pia alihangaika na tatizo hili, siku moja tukajaribu kumtafutia dawa ya asili(miti shamba),tangu amalize hiyo dawa hakuumwa tena ni miaka kama 15 imepita hasumbuliwi kabisa na hilo tatizo
Dawa gani ya asili nijuze mkuu na pia naweza kuipataje?? Msaada
 
Tafuta mkata vimeo akuangalie kimeo, kwa kawaida kikirefuka huwa nishida, mdogo wangu alikuwa na tatizo la hivyo hosp. alizungushwa zungushwa tuu ila mkata vimeo alifanya yake dogo hajawahi kusumbuliwa tena na vikohozi visivyo tibika!
 
utakuwa na vipele kwenye Koo, ndio maana hata ukila vitu vya baridi unakohoa, ukikaa kwenye chumba chenye AC napo ni shida.
 
Uwe unakaa ndani tu, maana ukitoka nje njiani ukikutana na hawa dada zetu halafu ukikohoa tu, utashtakiwa bure.
 
Mdogo wangu pia alihangaika na tatizo hili, siku moja tukajaribu kumtafutia dawa ya asili(miti shamba),tangu amalize hiyo dawa hakuumwa tena ni miaka kama 15 imepita hasumbuliwi kabisa na hilo tatizo
 
Ni ukweli mtupu nifuate inbox nitakuelekeza dawa ya kutumia bure na bila ya kukata, inshallah ndani ya wiki moja utakuwa umepona.
 
Tafuta mkata vimeo akuangalie kimeo, kwa kawaida kikirefuka huwa nishida, mdogo wangu alikuwa na tatizo la hivyo hosp. alizungushwa zungushwa tuu ila mkata vimeo alifanya yake dogo hajawahi kusumbuliwa tena na vikohozi visivyo tibika!
Maelezo zaidi huenda una matatizo ya moyo
Umri
Jinsia
Kazi yako
 
Mzee wangu badilisha maji unayokunywa, mm ilishawahi kunitokea, yaani nilizisha dawa za hospitali na pharmacy, ila kama mungu tu nikasema em niache kutumia aya maji ninayokunywa, nikawa natumia maji tofauti na yale niliokunywa mwanzo yaani kilipoa faster, alaf pendelea kula tangawizi inasaidia sana, kata kipande cha tangawizi tafuna inasaidia sna
 
Chronic cough kapime CT Scan ya kifua. Inaweza kua ni dalili za awali za saratani ya kifua. Fanya vipimo vikubwa.

Kila la heri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom