Nimepata kikohozi kisichoisha naomba msaada

Nimepata kikohozi kisichoisha naomba msaada

Tafuta Benylin. Hii ni dawa ya Dry Cough.

Bei yake ni kubwa kidogo lakini ni Nzuri sana iliweza kunisaidia sana. Maduka ya Jumla utaipata kwa 12000.
 
Tafuta Benylin. Hii ni dawa ya Dry Cough.
Bei yake ni kubwa kidogo lakini ni Nzuri sana iliweza kunisaidia sana. Maduka ya Jumla utaipata kwa 12000.
Asante kwa ushauri nitajaribu kuitafuta!!
 
Mdogo wangu pia alihangaika na tatizo hili, siku moja tukajaribu kumtafutia dawa ya asili(miti shamba),tangu amalize hiyo dawa hakuumwa tena ni miaka kama 15 imepita hasumbuliwi kabisa na hilo tatizo
Naomba uniambie hiyo daws tafadhali nahiyo shida hata mimi
 
Kuna mambo mawili yanaweza kuhusishwa:
1: Matatizo ya mzio/allergy
Hii inaweza kuwa ni tatizo, lakini pamoja na tiba unakuwa unaendelea kutumia vitu vinavyosababisha tatizo husika. Vitu hivyo ni kama: kutumia vitu vya baridi, feni, Ac, maji ya baridi au vinywaji, matumizi ya mafuta au pafyum zenye harufu kali, vyakula vyenye rangi zisizo za asili kama ubuyu wa rangi, juice za viwandani, maeneo yenye vumbi kwa wingi nk.

2: Uwezekano wa kuwa na acid reflux
Hii ni hali ya vitu vya tumboni kuweza kupanda na kuunguza njia ya chakula na kuathiri koo pia. Wakati mwingine hali hii huchanganywa na pumu. Kwa mazingira hayo kuna mambo yanahitajika kuzingatiwa pia pamoja na upataji wa tiba sahihi. Hivyo, kunakuwa na haja ya kuonana na daktari ili kutanabaisha ni nini hada tatizo.
 
Tafuta mkata vimeo akuangalie kimeo, kwa kawaida kikirefuka huwa nishida, mdogo wangu alikuwa na tatizo la hivyo hosp. alizungushwa zungushwa tuu ila mkata vimeo alifanya yake dogo hajawahi kusumbuliwa tena na vikohozi visivyo tibika!
Nyie nyie jamani si kutiana vilema tuuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom