hongera sana bi shost Zinduna Mungu akujalie kila la kheri na akulindie kibarua chako hicho .ni vizuri ukitoa shukrani kwenye nyumba yako ya ibada.na fungu la kumi katik amshahara wako.
Talk show unamuachia nani?
Baada ya kusotea ajira kwa takriban mwaka mzima, hatimaye jana nimeitwa na kusaini mkataba na kampuni hii iliyojikita hapa nchini kwa miaka kadhaa sasa. Kuanzia sasa nitakuwa ni mmoja wa waajiriwa wa kampuni hii inayojishughulisha na masuala ya utalii. Nitakuwa ni meneja wa ushauri na masoko kwa upande wa utalii katika kampuni hii ya Clouds Travel Agent yenye makao yake makuu visiwani ZNZ.....
Duh, sasa nitaanza kupokea mshahara.
Haya kina gfsonwin, cacico, amu, Asprin, Zion Daughter, Madame B, Ciello, charminglady, Arushaone, Mungi, Young Master, Preta, lara 1, BADILI TABIA, Kiranga, Bujibuji, Kaunga, Mamndenyi, King'asti, Erickb52, Ruttashobolwa, Fidel80, Bishanga, watu8, SnowBall, Mwita Maranya, figganigga, Preta, snowhite, @C6, marejesho, Lisa, nivea, Baba V, MadameX na wana chit chat wengine nawaomba msherehekee pamoja nami kwa kupata ajira!
Ciello, nitakualika uje Visiwani tule UROJO, TENDE na HALUA pale FORODHANI, kisha twen zetu pale Maeneo ya MAISARA katika Hoteli ya BAVUAI tupate PILAU na BIRIANI, nimeongea na meneja wa Hoteli hiyo Bwana Saidi kasema hatoniangusha, siku hiyo ukija atatuandalia Pilau la kukata na shokahahahahah ndomana yake...raha tujipe wenyewe lol
Ciello, nitakualika uje Visiwani tule UROJO, TENDE na HALUA pale FORODHANI, kisha twen zetu pale Maeneo ya MAISARA katika Hoteli ya BAVUAI tupate PILAU na BIRIANI, nimeongea na meneja wa Hoteli hiyo Bwana Saidi kasema hatoniangusha, siku hiyo ukija atatuandalia Pilau la kukata na shoka
ni mzuri sana best...na umetumia hekima kubwa. Inabidi twenzetu zenji lol wakati wengine wakienda tanga hahaha!!