excel
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 22,450
- 17,918
Niliona tangazo la kazi humu JF, nilituma mamombi na nikaitwa kwenye interview. Nilikuja kuomba ushauri hapa na watu wakafunguka vilivyo. Tulikuwa watu 46 nafasi zilikuwa 4. Namshukuru Mungu baada ya siku tatu nilitaarifiwa nimepata kazi.
Tayari nimeripoti eneo langu la mwezi wa pili sasa na hela ya kujikimu nimepewa 14 days kama kawaida maana ni taasisi ya UMMA.
Nashukuruni sana kwa msaada wenu.
mkuu tafadhali tujulishe yaliyojiri kwenye interview tafadhali!
maswali ya aina gani hasa yaliyoulizwa?
je, ulikutana na ugumu sehemu zipi wakati wa interview hasa ile ya oral?..bila kusahau na written!
how did you bargain the salary?
all in all, hongera kwa kupata kazi ndugu!!