Nimepata Chuo lakini nimekosa ada naomba Ushauri/Msaada

major2

Member
Sep 21, 2016
18
11
Habari wanajamvi,

Poleni na majuku,

Niko hapa kuomba ushauri.Nimebahatika kuchaguliwa Chuo kikuu Huria Tanzania kwa Masomo ya shahada ya Kwanza ya Sociology 2016/17.

Mpaka dakika hii sijapata ada na tarehe ya Kureport ni tarehe 4/12/2016.Naombeni ushauri wenu.Nifanyeje?

Epuka kukejeli au kuleta mzaha.
 
Pole kwa hilo, kabla ya kutaka kuendelea na masomo ulitegemea kupata hiyo ada wapi?
 
Kwa sasa una shughuli gani?? Kwa kuwa Open ni distance learning unaweza kutafuta Tempo akawa unafanya na unaendelea na kitabu, ama ufanye biashara ndogondogo uweze kupata fedha
 
Back
Top Bottom