Nimepata ajali ya bodaboda Kibiti

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,796
32,148
He'll

Katika kutimiza majukumu ya kazi leo nilikuwa Kibiti sehemu moja inaitwa mkamba nimetoka mjini saa nne nimefika saa nane mda ukawa umeenda sana na ilikuwa lazima kumaliza kazi leo sikutaka kulala uko

Nikawa nimemaliza kazi saa kumi na moja nikawa nauliza wenyeji usafiri wakaniambia boda buku mpaka kimanzi chana ndiko magari mengi huko pana umbali mrefu hapo nikasema poa nikawa nakula maandazi ya moto uku nangojea boda ya buku.

Kweli dakika sio nyingi ikaja boda nikasimamisha wenyeji wakawa wananiambia chini kwa chini komaa buku sawa nikafika pale nikawa nampanga boda boda anakataa buku ata 4000 nikamwambia nakupa 2000 akasema poa panda

Nikakwea boda kuanza kusepa duh tumeenda barabara ina mashimo boda ajali akanilusha juu nusu nianguke namwambia punguza mwendo sina haraka mimi asikii duh hatuja fika mbali mbele kuna gari af upande wetu kuna shimo vya barabarani

Nikiwa nimejawa hofu na mwendo wa boda boda bila kujali akapita vire vishimo kwq mwendo kasi nikarushwa tena nikasema kwa sauti subunaaall nikajikuta kwenye manyasi nilivaa msuli ili kuendena na culture za huko ule msuli nilio vaa ukafunguka naugulia maumivu nikabebwa pale kunipandisha kwenye boda boda.

Nikawa sasa nafoka namwambia boda nipeleke hospital nayo taka mimi akaniuliza pale wapi nika mjibu bochi au hindumental hospital baadae nikamuone huruma hapa kiuno kinauma kifua dah acha tu vitu vya bei poaa leo vimetokea puani​
 
Back
Top Bottom