Mtu anaweza kudhani ni story ya kutunga la la hasha, sina faida kwenye hilo, hiki ni kitu kinatokea kwa mara ya tatu Leo... Mida ileile
Baada ya kuota tena Leo, nimesita mno kuweka hili bandiko lakini kuna sauti inanisisitiza niandike..
Nimeota sijaoteshwa kuwa kuna mtu atakufa..... Lakini kila nikimwangalia namuona mwisho shingoni... Sura inanipotea na nikikazana kunyanyua macho yanapata kiza kisha nashtuka
Ndoto zipo za aina nyingi
Kuna ndoto kinyume
Kuna ndoto za wazi
Kuna ndoto taarifa
Kuna ndoto maono
Ndoto zenye tabia ya kujirudia rudia hizo ni ndoto taarifa ama maono... Watabiri wengi huzitumia sana hizi ndoto
Ndoto yangu pamoja na kujirudia lakini yaweza kuwa ndoto kinyume! Kwamba ukiota mtu atakufa basi itakuja kinyume chake kwamba kuna mtu atazaliwa
Lakini vilevile si lazima kiwe kifo cha roho kuachana na mwili, inawezekana ikawa mtu kuondolewa kwenye nafasi fulani kimadaraka ama mtu fulani kupata cheo kikubwa bila kutarajia (kumbuka vifo vingi sio jambo la kupanga)
Lakini pia inaweza kuwa na tafsiri ya mtu fulani kunusurika kifo au jambo lingine lolote baya... Ndoto nyingi hazina tafsiri moja, unachoangalia ni ile tafsiri inayoweza kuleta uhalisia zaidi kulingana na mazingira husika ya wakati huo
Ndoto ndoto hizi ukiwa muotaji sana halafu vitu unavyoota vikawa na uhalisia fulani kuna siku unaweza ukamwambia mtu WEWE UTAKUFA na akafa kweli
Kila ulalapo Mwombe sana Mungu kwa imani yako! Fanya dua, sali omba ndoto zako zitoke kwake na sio kuzimu.....