Nimeota Simba kashinda magoli mawili dhidi ya Nkana

Smt016

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
2,272
2,994
Kwanza kabisa nakiri ya kwamba mimi ni shabiki kindaki ndaki wa Yanga, sijawahi kuota ndoto juu ya tukio lihusulo mpira wa miguu. ila kwa mara yangu ya kwanza niliota ndoto kwenye mechi ya Ndanda vs Simba. Niliota ndoto simba kafungwa lakini mchezo ulimalizika kwa sare. Jana usiku ilikuwa ni mara yangu ya pili kuota ndoto juu ya tukio la mpira wa miguu na safari hii nimeota simba kashinda magoli mawili kwa bila dhidi ya Nkana.
 
Kwanza kabisa nakiri ya kwamba mimi ni shabiki kindaki ndaki wa Yanga, sijawahi kuota juu ya tukio lihusulo mpira wa miguu. ila kwa mara yangu ya kwanza niliota kwenye mechi ya Ndanda vs Simba. Niliota simba kafungwa lakini mchezo ulimalizika kwa sare. Jana usiku ilikuwa ni mara yangu ya pili kuota juu ya tukio la mpira wa miguu na safari hii nimeota simba kashinda magoli mawili kwa bila dhidi ya Nkana.
Umeota ukiwa mahindi au njugu mawe?
 
Mkuu kutesekea ni sehemu ya maisha. Kuna kipindi cha kutesa na kuteseka, "Kutesa kwa zamu"
We utakuwa mzalendo wa Nkana baada ya kuwa mzalendo wa Mbabane Swallows, ambapo mliangukia pua.

Kwa Simba hii. Mtateseka mno
 
Ha ha ha..kwahivyo mkuu unakubali Mnyama yuko juu ya Sheria kwa sasa eeeeh!!?
Ndio mkuu Kwa upande mmoja. ila kwa upande wa pili bado hawana hali nzuri sana maana Azam na Yanga hadi sasa naona breki zao zime fail kwahiyo wanaseleleka tu, ngoja tuone labda huu mseleleko ipo siku watagonga ukuta wa nyumba au ndio barabara itakuwa imenyooka hakuna bumps, wala kona hadi mwisho
 
Ndoto ya mwendawazimu
Kwani yeyote anayeota ndoto ni mwendawazimu? Ndoto ni ndoto, haijalishi tukio likatokea kweli au likatokea tofauti na lilivyokuwa kwenye njozi. Au ni kipi kilichokufanya unione mwandawazimu?
 
Kwanza kabisa nakiri ya kwamba mimi ni shabiki kindaki ndaki wa Yanga, sijawahi kuota ndoto juu ya tukio lihusulo mpira wa miguu. ila kwa mara yangu ya kwanza niliota ndoto kwenye mechi ya Ndanda vs Simba. Niliota ndoto simba kafungwa lakini mchezo ulimalizika kwa sare. Jana usiku ilikuwa ni mara yangu ya pili kuota ndoto juu ya tukio la mpira wa miguu na safari hii nimeota simba kashinda magoli mawili kwa bila dhidi ya Nkana.
Ndoto hiyo ipo kinyume chake,Nkana watawakalisha za kutosha tu maana golini mna pazia tu
 
Back
Top Bottom