Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,195
- 10,929
Pale kwenye njia ya reli kuelekea Gongo la mboto na kuendelea wamejenga tuta kuelekea upande wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKNI. Ujenzi unaendelea sijajua wataishia wapi au ndio wanaelekea uwanjani moja kwa moja?
Nimeuliza hivyo kwani natamani nione uwanja wa ndege wetu unaunganishwa na reli ya kisasa kama viwanja vya wenzetu. Ukiteremka kwenye ndege unaingia kwenye treni unaelekea mkoa unaotaka au unaingia Kisutu moja kwa moja.
Iwapo treni haitaingia uwanjani moja kwa moja basi angalau abiria akishatoka uwanjani anapanda lifti mpaka juu ya daraja anakokota mabegi yake mpaka upande wa pili wa barabara ama anasubiri treni yake au anasubiri gari za kumpeleka katikati ya jiji.
Uwanja wa JKNI mpaka sasa una eneo kubwa la bustani pamoja na kupendezesha macho lakini kuna matumizi bora zaidi kuliko hilo ili kuleta raha kwa wasafiri.