Nimeona bora nimuache aende tu

Nimeona bora nimuache aende tu

Huyu ni mpenzi wangu ambaye tumedumu kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja lakini sasa nasema baaaaasi.Kazidisha sana njaa ndomana nimeona bora nimuache aende.

Tabia kubwa ambayo inanikera na nimeivumilia mwishowe nimeshindwa ni kwamba unaweza mtumia pesa leo lakini baada ya siku mbili tu anakupiga mzinga mwingine sasa nabaki najiuliza ndani siku mbili anawezaje kutumia pesa bila mpangilio.

Kiukweli nimemvumilia sana tu ila sasa ngoja niwaachie wenye mpunga mnene huenda wakawezana nae ila kwangu mimi niseme tu imetosha.

Wanawake jifunzeni jinsi ya kuomba pesa, sio mtu anakutumia pesa leo baada ya siku mbili unaomba tena inamana unaemuomba yeye hana matumizi na pesa ama inakuaje.

Tukumbuke kwamba kila mtu ana maisha mengine nje ya mahusiano, kuna ndugu na jamaa nao wanahitaji msaada vilevile sio kwamba mwanamke tu ndo mwenye haki ya kutumia pesa za mpenzi wake.

Wacha awepelekee wengine sinema zake mimi kwangu imetosha.

Ukiona mwanamke anakuomba omba sanaa pesa sana jua hakupendi.
Pole
 
Back
Top Bottom