Nimeoa single mama

Nimeoa single mama

kibenten

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2018
Posts
499
Reaction score
510
Habarini wakuu,

Wiki hii nimeoa single mom, mtoto wake ana miaka 2 tangu azae jamaa alikimbia na hajulikani alipo hadi sasa hakutoa hata mia kwenye malezi ya mtoto, alisaidiwa kulea mtoto na mama yake, mtoto kamuacha kwao na mimi sitaki kuishi na huyo mtoto wake na yeye ashalikubali hilo maana tangu uchumba wetu wa mwaka mmoja, nishamwambiaga sitokaa na mtoto wako.

Ananipenda sana tena ile sana sijawahi kupendwa kama hivi kwa huu umri wangu wa 29 years nimewaacha wengi sana nimeamua yeye kumuoa nimeona hatasumbua kwa chochote maana ni mpole na msikivu sana.

Nimekuja tu humu kuwapa hiyo taarifa na kuja kuona mnaniusia wosia gani, kwa hiyo karibuni kwa maoni ya jinsi ya kuishi nae, na vitu gani nijitahadhari navyo, ushauri wowote pia unaruhusiwa na chochote ulichonacho cha kuniambia hata kiwe kibaya sawa tu karibu sana.
 
Siwezi na sitakuja weza kuishi na mtu akithubutu au kutamka au nikhisi anabagua mtoto wangu
Mtoto wangu kwanza
We hako katoto kanakupunguzia nin na watazaliwa ndugu zake hapo,ukishaamua kitu amua
Ukipenda boga penda na ua lake
 
habarini wakuu,,

wiki hii nimeoa single mom,mtoto wake ana miaka 2 tangu azae jamaaa alikimbia na hajulikani alipo hadi sasa hakutoa hata mia kweny malez ya mtoto,,alisaidiwa kulea mtoto na mama ake ,,mtoto kamuacha kwao na mi sitaki kuishi na uyo mtoto wake na yy ashalikubali hilo mana tangu uchumba wetu wa mwaka mmoja,nishamwambiaga sitokaa na mtoto wako.

ananipenda sana tena ile sana sijawahi kupendwa kama ivi kwa huu umri wangu wa 29 years,..nimewaacha wengi sana nimeamua yeye kumuoa nimeona hatasumbua kwa chochote mana ni mpole na msikivu sanaaaaaa.

nimekuja tu humu kuwapa hiyo taarifa na kuja kuona mnaniusia wosia gani,,,ko karibuni kwa maoni ya jinsi ya kuishi nae,,na vitu gan nijitahadhari navyo,ushauri wowote pia unaruhusiwa na chochote ulichonacho cha kuniambia hata kiwe kibaya sawa tu karibu sana.
Yaani watu wengine wame zaliwa na mikosi kwa 29yrs una oa single maza eti ana nipenda sanaa hiyo ni laana chunguza ukoo wenu nani ana kuroga
 
Siwezi na sitakuja weza kuishi na mtu akithubutu au kutamka au nikhisi anabagua mtoto wangu
Mtoto wangu kwanza
We hako katoto kanakupunguzia nin na watazaliwa ndugu zake hapo,ukishaamua kitu amua
Ukipenda boga penda na ua lake
Watazaliwa ndugu zake kwa kupitia Baba yupi maana mtoto hapo ana Baba mzazi na Baba mlezi
 
Siwezi na sitakuja weza kuishi na mtu akithubutu au kutamka au nikhisi anabagua mtoto wangu
Mtoto wangu kwanza
We hako katoto kanakupunguzia nin na watazaliwa ndugu zake hapo,ukishaamua kitu amua
Ukipenda boga penda na ua lake
Shida ni mawasiliano kuendelea na huyo baba wa mtoto,tumekaa nahudumia familia halafu inapigwa simu na mwanaume kuulizia hali ya mtoto ,ndiyo maana nasema kama sijaliona kaburi la baba yake na mtoto siwezi kuoa single mother.
 
Na mnaosemaga hivi ndio mnakujaga kuwaoa na kuwapenda sana
Usitukane mamba kabla hujavuka mto
 
Back
Top Bottom