Nimeoa mwanamke mkali naomba msaada nifanyaje

Nimeoa mwanamke mkali naomba msaada nifanyaje

Tafuta kaspring chicken ili kawe kanakufariji.
 
Miaka nenda rudi mpaka 9yrs ndo unamkwepa?!

Kama haikuwa tabia yake huko mwanzo lazima kuna tatizo
 
Mkuu nimekupa like kwa sababu we are sailing on the same sinking boat. nadhani wakulya ni bora kuolewa na wakulya wenzao its very hard to handle them. mi nimejitahidi kumbadilisha na kuongea naye kwa upole lakini naishia kutukanwa mpaka nimeamua option ya kukaa kimya na kutafakali nini cha kufanya.

Huyo mtwangwe kichapo cha nguvu utamuona atatulia Mkuu!! Unafanya kosa kubwa sana kukaa kimya!! Mtoe ngeu atakuheshimu!!
 
si kwamba nimemkimbia jumla hapana mda mwingi natumia kukaa Iringa peke yangu ni mdaa mchache ambao hauzidi siku kumi ndio tunakuwa wote lakini hizo siku kumi hawezi kukaa bila ugomvi.Kuhusu uvumilivu hiyo miaka tisa nimevumiliana sana nilipona nina miji wangu mwingine iringa nikaona isinipe shida heri kukaa peke yangu mda mwingi inamaana huko nyuma nilikuwa na nyumba moja tu mwanza nikawa navumilia ugomvi mda wote.kuhusu uamifu mimi ni mwaminifu sana sinywi pombe wala sina time na mademu.familia wanangu wote wako bording shuleni na ndio huniliwaza zaidi nao wanapendaa kukaa na mimi Iringa wanamuogopa mama yao sababu ya ukali wake.Kuhusu kuoa si unajua tena ndoa ya kikristo na nikifikili kuoa tena mke wa pili naona ndio yaleyale tu kutengeneza familia zisizo na mpango.Mda mwingi najalibu kujiweka bize na biashara zangu lakini bado najikuta naitaji msaada huyu mke nifanyaje? kupigana mimi sio mpenzi wa haya maisha maana nimekulia kwenye familia za kistarabu.
 
Mimi ni mfanyabiashara, nimemuoa mke wangu miaka tisa iliyopita kabila lake mkulya.Mke wangu ni mkali sana mpaka kwa wafanyakazi wetu wanaotusaidia kazi kiasi kwamba imebidi muda mwingi niwe nakaa peke yangu sababu ya kuepuka ugomvi usiokuwa na lazima.

Tumejenga nyumba mbili Mwanza na Iringa najikuta mda mwingi nautumia kukaa peke yangu Iringa ili kuepuka ugomvi usiokuwa na maana ingawa yeye hajui kwa nini lakini bado atapiga simu mtagombana na ndoa yangu ya kikristo.

Wanajamvi nifanyaje?


Kuna uwezekano mkeo anakuona zoba ndio maana anakuwa mkali....be a man and show leadership....man up
Acha kulalama utadhani mke ulienae ni wa urithi.
 
Muraaaaaa! Acha swaga zenu Za mjini mbane,Sio mkulya ni mkurya,Arooooo mghuuu pande,Mghuuuu Sawa,Uighure?::
 
Pga chini oa mpole. Gawaneni nyumba maisha yaendlee. Ndoa ya kikristo ndo nini bwana! Aliyekufungsha ndoa naye ana kademu pembeni
 
aisee shukuru mungu,mwanamke mkali anajua sana kuhandle nyumba,ungepata mpole kama wachaga wa uru ungelia,bila shaka mgeishaachana.
 
Pole sana! Wanawake wengi ndivyo walivyo, ni walemavu kwa hiyo ulioa mlemavu, hivyo unatakiwa kuiishi hali hiyo mpaka kifo, huo ni ulemavu sawa tu na mtu akiwa taahira au kiwete huwezi kusema huyu ni kiwete sasa namwacha; jitahidi kujifanyia mambo yako muhimu maadam humbebi mgongoni muda mwingi mwaache awe na maisha yake akitukana unaka kimya, akipiga kelele kama radi unakaa kimya; usijibizane na kichaa. Nilifanya hivyo nilifanikiwa saaaaaaaaaaaaana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom