Zemanga zoze
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 990
- 1,637
Leo nikiwa katika mihangaiko yangu ya kila siku muda wa saa, saba mchana nilipigiwa simu na jamaa yangu tuliyesoma nae shule ya upili, rafiki yangu huyu yeye ni boda boda na alinipa taarifa kwamba mama yake ni mgonjwa hivyo nikaona ni vizuri nipite kumjulia hali.
Akanielekeza sehemu anayo tafutia riziki nikaenda, baada ya kufika tukawa tunapiga stori kidogo kabla hatujaelekea kwao kumuona mama yake.
Ghafla tuu tukajikuta tuko chini tumepigwa mitama na polisi, mara makofi bakora vibao ukiuliza kosa unapigwa vibaya mno tukakamatwa na wenzetu kama nane tukawekwa ndani ya gari ,huku tukiendelea kukanyagwa virungu vingi vikiendelea kutembea.
Tulipofika kituoni, tukaambiwa kuna mauaji yametokea mtaa wa pili jana usiku sa sita kwahiyo tunahitajika tutoe ushirikiano wa kupatikana kwa mtuhumiwa mmoja aliyehusika ambae anasemekana anakaa mitaa hiyo.
Tulipofika kituoni tukachukuliwa maelezo tukaswekwa rumande, tumekaa masaa sita tukiugulia maumivu huku kunguni, chawa, papasi wakiendelea kututafuna, tunashukuru nguvu za ndugu na majirani kuandamana mpaka kituoni kutetea haki zetu tumekuja kutoka saa moja na nusu usiku.
Kwa utaratibu huu kweli jeshi la polisi liko kwa ajili ya kulinda usalama wa raia au kukandamiza na kudhalilisha raia tunashukuru tumetoka japo kuna wenzetu wamebaki inasikitisha sana.