Nimenusurika kubambikiwa kesi ya mauaji leo kituo kikuu cha Polisi Dodoma

Zemanga zoze

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
990
1,634
Leo nikiwa katika mihangaiko yangu ya kila siku muda wa saa, saba mchana nilipigiwa simu na jamaa yangu tuliyesoma nae shule ya upili, rafiki yangu huyu yeye ni boda boda na alinipa taarifa kwamba mama yake ni mgonjwa hivyo nikaona ni vizuri nipite kumjulia hali.

Akanielekeza sehemu anayo tafutia riziki nikaenda, baada ya kufika tukawa tunapiga stori kidogo kabla hatujaelekea kwao kumuona mama yake.

Ghafla tuu tukajikuta tuko chini tumepigwa mitama na polisi, mara makofi bakora vibao ukiuliza kosa unapigwa vibaya mno tukakamatwa na wenzetu kama nane tukawekwa ndani ya gari ,huku tukiendelea kukanyagwa virungu vingi vikiendelea kutembea.

Tulipofika kituoni, tukaambiwa kuna mauaji yametokea mtaa wa pili jana usiku sa sita kwahiyo tunahitajika tutoe ushirikiano wa kupatikana kwa mtuhumiwa mmoja aliyehusika ambae anasemekana anakaa mitaa hiyo.

Tulipofika kituoni tukachukuliwa maelezo tukaswekwa rumande, tumekaa masaa sita tukiugulia maumivu huku kunguni, chawa, papasi wakiendelea kututafuna, tunashukuru nguvu za ndugu na majirani kuandamana mpaka kituoni kutetea haki zetu tumekuja kutoka saa moja na nusu usiku.

Kwa utaratibu huu kweli jeshi la polisi liko kwa ajili ya kulinda usalama wa raia au kukandamiza na kudhalilisha raia tunashukuru tumetoka japo kuna wenzetu wamebaki inasikitisha sana.
 
Sidhani kama inawezekana,yaani mkusanywe tu kiboyaboya kwa mauaji ya mtu asiyejulikana hapo mtaani wakati waliompiga risasi lissu mpaka Leo hawajakamatwa
 
Yeah inawezekana kabisa,
Huyo victorie atakua ni polisi na vyeo vyake au yupo kwenye sekta nyeti nyeti kwaiyo usimbishie
Marais, Majaji, Majenerali wa Jeshi, Mabosi wa Intelligence Agencies, Makamishina wa Polisi, Wafanyabiashara na Matajiri Wakubwa, Viongozi wa Dino, na wengine wengi kama hao, nao hawajawahi kukwepa "kunyea debe"! Sasa huyo Victoire atakuwa kwenye sekta ipi kwenye dunia hii hadi afikie kuapa "never ever" atakuja kulala polisi maishani make?!
 
Marais, Majaji, Majenerali wa Jeshi, Mabosi wa Intelligence Agencies, Makamishina wa Polisi, Wafanyabiashara na Matajiri Wakubwa, Viongozi wa Dino, na wengine wengi kama hao, nao hawajawahi kukwepa "kunyea debe"! Sasa huyo Victoire atakuwa kwenye sekta ipi kwenye dunia hii hadi afikie kuapa "never ever" atakuja kulala polisi maishani make?!

Atakua na uwezo usio wa kawaida jini 😂
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom