Nimemuuliza tu!kawa mkali kama pilipili

Nimemuuliza tu!kawa mkali kama pilipili

kokudo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
2,571
Reaction score
1,784
Nilimpigia simu nikaikuta inatumika nikakata nikijua akimaliza atanitafuta hakunitafuta nilivyokuja kupiga akaniambia anatoka kuoga nikamuuliza mbona simu yako ilikua inaongea?duh kawa mkali mpaka mahusiano yanakaribia kuvunjika

Je ni vibaya kuuliza kama unahisi ndivyosivyo ili usionekane mfatiliaji sana au uonekane mzungu usiejari mambo hayo?
 
Kuna trafiki alikuwa anamuuliza driving license, hakuwa nayo akapigwa bao!
 
Wala hakujali huyo
Anamjali mwingine
 
Yaani vitu vidogo kama kutojibiwa/kutopigiwa sm navyo vikufanye uwehuke? Nilidhani utasema ulifika mlangoni ukakuta umebanwa kwa ndani na minong'ono humo. Ukaondoka ukarudi kuuliza ukawasha moto.
Kumbe sm ilikuwa bize? Hata alikustahi kukuambia alikuwa bafuni. Ulitaka aseme na weye na sabuni machoni? Akitoka na macho mekundu ungesemaje? Mwache mwenzio apumueeeeeeee
 
Mmmh,hapo kuna tatizo ila usimuhukumu kwanza fanya uchunguzi bila ya yy kujua utapata jibu.
 
Nilimpigia simu nikaikuta inatumika nikakata nikijua akimaliza atanitafuta hakunitafuta nilivyokuja kupiga akaniambia anatoka kuoga nikamuuliza mbona simu yako ilikua inaongea?duh kawa mkali mpaka mahusiano yanakaribia kuvunjika
Je ni vibaya kuuliza kama unahis ndivyosivyo ili usionekane mfatiliaji sana au uonekane mzungu usiejari mambo hayo?

kwanza kama hana asili ya ukali bas jua
his not that into you
kama ana asili ya ukali yan mtu wa kureact vitu vidogo mzoee
 
Inategemea ulimpigia simu saa ngapi...
Ingekuwa usiku mnene hapo unaweza kuuliza.

Pia sio simu zote zinazoonyesha namba (missed callz) wakati inatumika.

Usilaumu yawezekana hakuona kama ulimtafuta.
 
Yaani vitu vidogo kama kutojibiwa/kutopigiwa sm navyo vikufanye uwehuke? Nilidhani utasema ulifika mlangoni ukakuta umebanwa kwa ndani na minong'ono humo. Ukaondoka ukarudi kuuliza ukawasha moto.
Kumbe sm ilikuwa bize? Hata alikustahi kukuambia alikuwa bafuni. Ulitaka aseme na weye na sabuni machoni? Akitoka na macho mekundu ungesemaje? Mwache mwenzio apumueeeeeeee

Haya ni wazo zuri
 
..mimi nikipiga simu mara moja kama inatumika uwa napiga tena kwa mara ya pili na ya tatu mana muda mwingine unaambiwa simu inatumika ila ukipiga tena muda huohuo inaita nadhani ni matatizo ya mtandao...Kuhusu kuwa mkali jaribu kuchunguza mambo mengine labda kuna vitu haviko sawa ndo mana ni mkali...
 
Inategemea ulimpigia simu saa ngapi...
Ingekuwa usiku mnene hapo unaweza kuuliza.

Pia sio simu zote zinazoonyesha namba (missed callz) wakati inatumika.

Usilaumu yawezekana hakuona kama ulimtafuta.

Anyway inaweza kua
 
..mimi nikipiga simu mara moja kama inatumika uwa napiga tena kwa mara ya pili na ya tatu mana muda mwingine unaambiwa simu inatumika ila ukipiga tena muda huohuo inaita nadhani ni matatizo ya mtandao...Kuhusu kuwa mkali jaribu kuchunguza mambo mengine labda kuna vitu haviko sawa ndo mana ni mkali...

Asante sister but nilivyokuta iko inatumika nilikata badae nikapiga akadai alikua bafuni hapo ndo utata mh may be netwark sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom