Nimemuelewa Halima Mdee. Amekubali makosa, anataka maridhiano; yuko tayari kujirudi na kurekebisha mambo chamani mwao

2010 Dr Slaa si aliibiwa kura?
2015 Lowassa si aliibiwa kura?

Mara zote hizo waliingia Bungeni.

Kwanini safari hii formula ibadilike kwa kuwa tu Wanaume wote hawatakuwa wabunge?

Ajabu kuwa huyu ni mwanasheria lakini alishau kabisa jambo muhimu la kumshitumu mtu - ushahidi. Huyu bibi alisema ameona kwa macho yake karatasi feki za kara katika jimbo lake. Lakini akiwa kama mwanasheria alishindwa kuwashirikisha askari au kuchukuwa ushahidi na kuufikisha kwa NEC, polisi au hata mahakamani. Ajabu sana hakuja na picha au clip zake yeye binafspamoja na hizo karatasi, hakuja na majina ya watu waliokuwepo huko alikozikuta hizo karatasi feki ila alikuja ma neno tu. Halafu sasa anageuka na kukubali kufanya kazi na wale wale aliowaita wezi.
 
Leo, kama mtanzania wa kawaida nisiye mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini na kwingineko, nimepata bahati ya kumsikiliza Mhe. Halima Mdee aliyekuwa mzungumzaji mkuu kwenye mkutano wao na waandishi wa habari...
Kwa jinsi tu ulivyoaanza na kujitetea kuwa sio Mwanachama wa chama chochote (jambo ambalo halikuwa na msingi wowote) tayari werevu tulishajua nini kitakachofuata katika andiko lako Mzee wa Lumumba.

Hakika sijasoma andiko lako loote hasa baada ya kusoma utangulizi. lakini kiufupi Halima Mdee leo kajivua nguo na kawaondolea mashaka kabisa watanzania wengi waliokuwa wanashindwa kujua kama kasaliti au alikuwa na nia njema.

Kwa ufupi kaharibu saana ni bora angeendelea kujificha huku alipokuwa amefichwa pengine ingesaidia kwa wananchi kuendelea kuumiza vichwa vyao juu ya nini ilikuwa adhima yake na kundi lake
 
Pili, Katiba na Sheria haziwezi kuzidiwa nguvu na kauli ya yeyote yule ndani au nje ya Tanzania.
Mbona mara kadha imezidiwa na walio na mabunduki na mabomu..., mbona watu mnapenda sana kujipumbaza kwa vitu mnavyojua kwa uhakika vipo?

Huto tu sheria twenu tutasaidia nini iwapo huo mhimili mnaoutegemea nao ulishatekwa?
 
2010 Dr Slaa si aliibiwa kura?
2015 Lowassa si aliibiwa kura?

Mara zote hizo waliingia Bungeni


Kwanini safari hii formula ibadilike kwa kuwa tu Wanaume wote hawatakuwa wabunge?
Kosa la kina halima ni kuwa na haraka, kwa vile chama Chao hakikupitisha mchakato wa viti maalumu walipaswa kusubiri ama kujenga hoja kamati kuu ili waruhusiwe kwenda bungeni.kosa lao ni kilazimisha
 
Kwa hiyo Mdee bado anaweza kurudi bungeni pale rais akiamua kumchagua kuwa miongoni mwa watu 10 anaoruhusiwa kuwachagua? au ni lazima watu k10 amaowachagua raisi ni lazima watoke katika chama tawala?
Anaweza. Rais Mstaafu Kikwete aliwahi kumteua Mhe Mbatia akiwa si MwanaCCM. Na nimeeleza kuhusu hilo kwenye mada yangu
 
Nafikiri katoa Maelezo mazuri ya kueleweka na kukubali kuwa wamefukuzwa na si wanachama wa chadema.

Kauli hii naimithirisha na upepo mkubwa wa kuweza kuinua lilekoti la muapishaji na kumfunika usoni huku likiacha aibu zake wazi. Nafikiri muapishajj achutame tusiendelee kuona mambo yake ni aibu.
 
Leo, kama mtanzania wa kawaida nisiye mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini na kwingineko, nimepata bahati ya kumsikiliza Mhe. Halima Mdee aliyekuwa mzungumzaji mkuu kwenye mkutano wao na waandishi wa habari..
Imani yangu ni kuwa Mdee hakuwa mtu wa kukisaliti chama chake,ila kuna msukumo kutoka mahaloi fulani penye manguvu ya kutisha imepelekea Halima na kundi lake kujikuta hapo walipo.
 
Hapo kuweka mambo sawa ni wao kujiuzulu kwanza kwakuwa wamekiri hawakufuata taratibu za chama. Kama mchakato wa kuteua wabunge wengine wa viti maalumu utafuata sheria na kanuni za chama.

Lakini kuendelea kuwa mbunge huku anasema anaipenda CHADEMA ni kuwahadaa wanachama na wapenzi wa CHADEMA ama kuendekeza njaa tu
Kujiuzulu kunatoka wapi tena wakati wameshavuliwa uanachama wa chama chao cha zamani, CHADEMA...?

Wanachotakiwa kufanya kama alivyoshauri mleta mada ni wao kupatana na chama chao ili maamuzi yawe reversed jambo ambalo ni gumu kidogo kutendeka...

Baada ya hapo watoe hizo hoja walizozitoa leo, wazungumze ndani ya chama wakielewana, basi wanaweza kuteuliwa tena kuwa wabunge japo hili ni gumu sana kulingana na msimamo wa CHADEMA kutoyatambua matokeo yote ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 ya kuwa ni batili...!!
 
Hakuna mapatano hapo,hao wameshageuka mamluki ,imani walisha ipoteza.

Hapana, kupatana kwa upande mmoja kunawezekana under one condition.

Wakubali kuwa walikengeuka na kukosea. Hii ndiyo dawa ya mapatano. Kukiri kosa na kuomba msamaha.

On the other hand ni ngumu kwa sababu walishaonja vya shetani. Inawezekana kuwa rahisi iwapo watamkataa shetani na kazi zake zote...!!

Who is shetani? I hope you know.
 
2Barua inaelekezwa kwa spika, tayari kajitoa fahamu na kuwatangazia ulinzi wabunge 19. Amewahakikishia ni wabunge halali
[/QUOTE]
Kama taifa tunashida kubwa ambayo hata sisi wenyewe hatujui kama ni tatizo.
 
Kwa jinsi tu ulivyoaanza na kujitetea kuwa sio mwanachama wa chama chochote (jambo ambalo halikuwa na msingi wowote) tayari werevu tulishajua nini kitakachofuata katika andiko lako Mzee wa Lumumba...
Soma, ni andiko fupi la kumaliza ndani ya muda mfupi. Usimchukulie kwa mazoea
 
Leo, kama mtanzania wa kawaida nisiye mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini na kwingineko, nimepata bahati ya kumsikiliza Mhe. Halima Mdee aliyekuwa mzungumzaji mkuu kwenye mkutano wao na waandishi wa habari...
Rule of law should be a cornerstone of our nation! Even the persons that have the power to be above the law by instruments, should observe the existence of such instruments as the law itself !

Wenye mamlaka wasitumie mapungufu ya kisheria yanayotoa mianya ya ubabe kuwa wababe. Huo ni ushamba uliopitiliza.
 
Kwa jinsi tu ulivyoaanza na kujitetea kuwa sio mwanachama wa chama chochote (jambo ambalo halikuwa na msingi wowote) tayari werevu tulishajua nini kitakachofuata katika andiko lako Mzee wa Lumumba...
Umeamua na kuchangia vyema mawazo yako. Lakini, kauli ya kutokuwa na chama ni muhimu kwangu kuonyesha jinsi nisivyolalia upande wowote kisiasa. Ubarikiwe sana!
 
Umeamua na kuchangia vyema mawazo yako. Lakini, kauli ya kutokuwa na chama ni muhimu kwangu kuonyesha jinsi nisivyolalia upande wowote kisiasa. Ubarikiwe sana!
Tatizo Mkuu umeanza kujitetea kabla ya hujahukumiwa na watakaosoma andiko lako exactly kama alivyofanya Halima leo kwa kusema eti hajaongwa sijui mambo ya watu wakaangalie akaunti yake benki huku akisahau kuwa wananchi wanajua kila kitu kuhusu nini anacholipwa Mbunge bila kujali ni wa viti maalum au wakuchaguliwa..
 
Back
Top Bottom