Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Leo, kama Mtanzania wa kawaida nisiye mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini na kwingineko, nimepata bahati ya kumsikiliza Mhe. Halima Mdee aliyekuwa mzungumzaji mkuu kwenye mkutano wao na waandishi wa habari.
Mhe. Mdee alikuwa mzungumzaji mkuu wa waliofukuzwa uanachama wa CHADEMA. Ni wale 19 walioapishwa kama Wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA. Nimemsikiliza na kumuelewa. Unataka maridhiano, anataka amani na upatano ndani ya CHADEMA.
Kwakuwa Mhe. Mdee ni Mwanasheria kama mimi, ni wazi kuwa anajua mambo yafuatayo. Mosi, Katiba ya Tanzania ni sheria mama na ni lazima matakwa ya kikatiba yalindwe na kutekelezwa. Pili, Katiba na Sheria haziwezi kuzidiwa nguvu na kauli ya yeyote yule ndani au nje ya Tanzania.
Tatu, kwamba kuna aina za Wabunge wafuatao: (i) Wabunge wa Majimbo (ii) Wabunge wa Viti Maalum (iii) Wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais (iv) Wabunge watano wanaochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwao (v) Mwanasheria Mkuu wa Serikali (vi) Spika wa Bunge kama hatokani na Wabunge.
Nne, ni Wabunge 10 tu wanaoteuliwa na Rais pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiyo ambao si lazima wapendekezwe na kudhaminiwa na chama cha siasa katika kupatikana kwao. Waliobakia ni lazima wapendekezwe na kudhaminiwa na chama cha siasa katika kupatikana kwao na kuwa Wabunge.
Tano, iko wazi kikatiba (na haijalishi kauli ya yeyote yule) kuwa Mbunge anapopoteza uanachama wa chama kilichompendekeza na kumdhamini, ubunge wake hukoma pia. Hivyobasi, kwa kufukuzwa uanachama wao (kwakuwa uamuzi wa CHADEMA bado haujabadilishwa au kubadilika) Mhe. Halima Mdee na wenzake 18 walikoma kuwa Wabunge kikatiba na kisheria.
Sita, ubunge wa Viti Maalum una mchakato na utaratibu wake wa kikatiba, kisheria na kiutaratibu wa ndani ya vyama husika. Na kwamba Katiba, sheria na taratibu lazima zifuatwe ili kuhalalisha ubunge huo.
Kiukweli, namsifu Mhe. Halima Mdee kwa kuzungumza kwake kwa staha, busara na hekima kubwa hasa kuhusu chama chake cha zamani CHADEMA na viongozi wake. Najua bila shaka kuwa Mdee na wenzake wanajua taratibu za kufuata ili kuubadili uamuzi wa CHADEMA ndani na nje ya chama hicho.
Kwa ilivyo sasa, Mhe. Halima Mdee na wenzake 18 ambao wamefukuzwa uanachama wa CHADEMA, kikatiba na kisheria, si Wabunge. Kwa busara na staha walioionyesha Leo, wapewe nafasi ya kurekebisha mambo ndani ya CHADEMA na kusonga mbele pamoja!