dalloboy
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 314
- 246
Mambo vipi wadau,
Naomba nielekee moja kwa moja kwenye mada yenyewe. Ni kwamba nimedumu katika uhusiano na mpenzi wangu takribani 3 years. Niseme ukweli katika mahusiano yangu yaliyopita sijawahi kudumu muda mrefu kiasi hicho, kwahiyo inamaana nilimpenda sana tena zaidi ya sana.
Yeye pia hakuwa nyuma kunionesha upendo wa dhati. Nakiri wazi alinipenda pia sana, japo matatizo madogo madogo katika uhusiano huwa hayakosi. Nasikitika kuanzia leo sitoshiriki nae baadhi ya vitu kama hapo zamani.
Niende kwenye inshu yenyewe ambayo imenifanya nimuache huyu mlimbwende wangu. Ni kwamba mimi katika mahusiano yetu nilikuwa nasisitiza sana juu ya kupata mtoto. Napenda mtoto, napenda niitwe baba.
Ikumbukwe huyu manzi alikuwa anasoma na hapa juzi ndo kamaliza form six na tuliahidiana nimsubiri mpaka amalize six then taratibu za kupata mtoto zianze. Lakini leo hii nimegeukwa, nimekuwa nikimkumbusha juu ya ahadi yetu lakini ananizungusha tu mpaka nilipombana na kutaka kujua iwapo atanizalia au hawezi.
Nasikitika alinijibu kuwa anaogopa sasa hivi kuzaa hivyo nimvumilie eti mpaka amalize chuo. Nimeumia sana, sio siri nilijihsi vibaya sana. Kwanini hakuniambia siku zote kwamba hawezi kunizalia basi nikae najua kuliko kunidanganya hivyo?
Nimemuacha,na maisha yake japo amelia sana juu ya kuvunjika kwa uhusiano wetu lakini siwezi kurudi nyuma tena.
Kwaheri mama kwaheri!