Nimemuacha mpenzi baada ya kushindwa kunizalia

dalloboy

JF-Expert Member
May 31, 2016
314
246
Mambo vipi wadau,

Naomba nielekee moja kwa moja kwenye mada yenyewe. Ni kwamba nimedumu katika uhusiano na mpenzi wangu takribani 3 years. Niseme ukweli katika mahusiano yangu yaliyopita sijawahi kudumu muda mrefu kiasi hicho, kwahiyo inamaana nilimpenda sana tena zaidi ya sana.

Yeye pia hakuwa nyuma kunionesha upendo wa dhati. Nakiri wazi alinipenda pia sana, japo matatizo madogo madogo katika uhusiano huwa hayakosi. Nasikitika kuanzia leo sitoshiriki nae baadhi ya vitu kama hapo zamani.

Niende kwenye inshu yenyewe ambayo imenifanya nimuache huyu mlimbwende wangu. Ni kwamba mimi katika mahusiano yetu nilikuwa nasisitiza sana juu ya kupata mtoto. Napenda mtoto, napenda niitwe baba.

Ikumbukwe huyu manzi alikuwa anasoma na hapa juzi ndo kamaliza form six na tuliahidiana nimsubiri mpaka amalize six then taratibu za kupata mtoto zianze. Lakini leo hii nimegeukwa, nimekuwa nikimkumbusha juu ya ahadi yetu lakini ananizungusha tu mpaka nilipombana na kutaka kujua iwapo atanizalia au hawezi.

Nasikitika alinijibu kuwa anaogopa sasa hivi kuzaa hivyo nimvumilie eti mpaka amalize chuo. Nimeumia sana, sio siri nilijihsi vibaya sana. Kwanini hakuniambia siku zote kwamba hawezi kunizalia basi nikae najua kuliko kunidanganya hivyo?

Nimemuacha,na maisha yake japo amelia sana juu ya kuvunjika kwa uhusiano wetu lakini siwezi kurudi nyuma tena.

Kwaheri mama kwaheri!
 
Mambo vp wadau " naomba nielekee moja kwa moja kwenye mada yenyewe.... Ni kwamba nmedumu katika uhusiano na mpenzi wangu takribani 3 years " niseme kwel katika Mahusiano yangu yaliopita sijawahi kudumu mda mrefu kiasi hicho, kwahiyo inamaana nilimpenda sana tena zaidi ya sana, na ye pia hakuwa nyuma kunionesha upendo wa dhati nakiri wazi alinipenda pia sana, japo matatizo madogo madogo katika uhusiano huwa hayakosi , naskitika kuanzia leo sintoshiriki nae baadhi ya vitu Kama hapo zamani. Niende kwenye inshu yenyewe ambayo imenifanya nimuache huyu mlimbwende wangu ni kwamba mimi katika Mahusiano yetu nilikuwa nasistza sana juu ya kupata mtoto napenda mtoto, napenda niitwe baba , ikumbukwe huyu manzi alikuwa anasoma na hapa juzi ndo kamaliza form six, na tuliahidiana nimsubiri mpaka amalize six then taratibu za kupata mtoto zianze " lakini leo hii nmegeukwa nmekuwa nikimkumbusha juu ya ahadi yetu ananizungusha tu mpaka nilipombana na kutaka kujua iwapo atanizalia au hawezi, naskitika alinijibu kuwa anaogopa sasa hivi kuzaa hivyo nmvumilie et mpaka amalize chuo , nmeumia sana sio siri niljhsi vibaya sana, kwanini hakuniambia siku zote Kama hawezi kunizalia basi nikae najua kuliko kunidanganya hivyo, nmemuacha, nmemuacha na maisha yake' japo amelia sana juu ya kuvunjika kwa uhusiano wetu lakini siwezi kurudi nyuma tena " kwaheri mam.... kwaheri.......
Unakimbilia mtoto badala ya ndoa,muoe mtoto wa watu uwone km atashindwa kukuzalia,alafu nyie wanaume baadhi yenu ndo mlivyo mimi mwenyew yalinishida hayo hayo mtu ana kazania mtoto ukimwambia khs ndoa ana kwepa lol
 
Yani hawa ndugu zetu, uishi nao kwa akili sana. Wengine atajishaua hadi kulia eti anataka mtoto, beba mimba uanze kuona nyota nyota. Wengine hadi mahari wamelipiwa, wakajua wamefika so wakabeba mimba, kalagabaho
 
Mambo vipi wadau,

Naomba nielekee moja kwa moja kwenye mada yenyewe. Ni kwamba nimedumu katika uhusiano na mpenzi wangu takribani 3 years. Niseme ukweli katika mahusiano yangu yaliyopita sijawahi kudumu muda mrefu kiasi hicho, kwahiyo inamaana nilimpenda sana tena zaidi ya sana.

Yeye pia hakuwa nyuma kunionesha upendo wa dhati. Nakiri wazi alinipenda pia sana, japo matatizo madogo madogo katika uhusiano huwa hayakosi. Nasikitika kuanzia leo sitoshiriki nae baadhi ya vitu kama hapo zamani.

Niende kwenye inshu yenyewe ambayo imenifanya nimuache huyu mlimbwende wangu. Ni kwamba mimi katika mahusiano yetu nilikuwa nasisitiza sana juu ya kupata mtoto. Napenda mtoto, napenda niitwe baba.

Ikumbukwe huyu manzi alikuwa anasoma na hapa juzi ndo kamaliza form six na tuliahidiana nimsubiri mpaka amalize six then taratibu za kupata mtoto zianze. Lakini leo hii nimegeukwa, nimekuwa nikimkumbusha juu ya ahadi yetu lakini ananizungusha tu mpaka nilipombana na kutaka kujua iwapo atanizalia au hawezi.

Nasikitika alinijibu kuwa anaogopa sasa hivi kuzaa hivyo nimvumilie eti mpaka amalize chuo. Nimeumia sana, sio siri nilijihsi vibaya sana. Kwanini hakuniambia siku zote kwamba hawezi kunizalia basi nikae najua kuliko kunidanganya hivyo?

Nimemuacha,na maisha yake japo amelia sana juu ya kuvunjika kwa uhusiano wetu lakini siwezi kurudi nyuma tena.

Kwaheri mama kwaheri!
Sasa wewe maandishi yako tu yanaonesha ni mwandiko wa kitoto, sasa mtoto unapotaka kuwa kuwa na mtoto huoni hili ni tatizo? Kwanza inaonesha wazi wewe bado unahitaji malezi ya wazazi wako na ya kiroho ili uelewe hata kwenye amri 10 za Mungu inayosema usidhini pia usitamani mwanamke asiyekuwa mke wako.

Wewe ulimuoa lini huyo binti wa watu mpaka uanze mjadala wa uzazi? Wasichana wote mnaosoma thread hii mjiepushe na wavulana wa aina hii.
 
Kwa hiyo mkaahidiana mpaka amalize form six ndo abebe mimba, inamaana ulimuomba akubebe mimba tangu akiwa 0 level na akakutolea nje akakuambia usubiri mpaka amalize six? Mahari ushatoa kwanza? Alafu hiyo five na six umemlipia ada wewe au wazazi wake? Wewe mwanaume wa wapi wewe? wezio ndo tunawatia moyo wasome angalau wajue dunia wewe mtoto kamaliza six hata matokeo bado unataka mimba? alafu unauita huu ndo upendo? au elimu yako ya kuunga unga unaona kuwa akipiga kitabu mpaka chuo kikuu nyumbani hakutakalika?

NAMSHAUri huyo demu akuogope na akukimbie kama ebola. Hapo ukishamtia kitu ndo shule basi tena, anakuwa mama wa nyumbani mwenye elimu ya kidato cha sita.
 
Kama ulikuwa una dyudyu nae imekushindaje kumuweka mimba? Tatizo sio demu naona wewe ndio unalo tatizo yaani unaweka wese kwenye gari lakini kuendesha hujui??
 
Daaaaah kuna watu mmewageuza mademu zenu kama kuku wa mayai azae pale unapokisikia na sio makubaliano ya ndo,
Unataka akuzalie matiti yakilala nanharufu za mwanao umkimbieee, nyambafu sana mi nikajua umemwambia swala la kufunga ndoa ndio akakwambia usibiri atoke chuo?? Kumbe unataka kua unahesabu idadi ya watoto hata matunzo hujui gharama hata ya kidaso ili uwe unampost fb, jinga sana wanaume wenye mawazo kama yako na Mungu awape wakina dada roho ya utambuzi wa majizi ya ndoto zao.

We unadai uzaliwe mtoto alipodai ndoa majibu hujatwambia ulimjibu nini??? Kama unapenda watoto wa bila majukumu nenda kawaangilie huko fb

Hutaki majukumu halafu unataka jina la jukumu shenzi kabisaaa

Huyo dada hiyo itakua kinga yake dhidi ya wote wenye nia mbaya kama yako

Namshauri asiumie kwani kuna msemo usemao
"" kuishi na mpenzi mda mrefu halafu mkaachana anakuachia shule ya kuishi na mwenza wako wa milele""
 
Una hamu ya kuitwa baba si uoe uzae eishhh. Hako kabinti kanalia tu sasa hivi, ila baadaye katamshukuru sana Mungu kwa ufahamu aliompa. Kesho an Kesho kutwa wa kwanza kuwasema "baby mommas"
Ukiona mwanaume anataka mtoto kabla ya ndoa ujue hakupendi...
Yani hawa ndugu zetu, uishi nao kwa akili sana. Wengine atajishaua hadi kulia eti anataka mtoto, beba mimba uanze kuona nyota nyota. Wengine hadi mahari wamelipiwa, wakajua wamefika so wakabeba mimba, kalagabaho
 
kesi yenu ina mambo mengi ya kusiikilizwa..
katika nyanja tofauti tofauti
ili kila mtu apate usawa...

haya hongereni kwa kuachana...
welcome back into the world of hoeing....
 
Nadhani wapo waliojigrade kama mitambo ya kufyatulia watoto, na utawasikia wenyewe wakitamba lazima nimzalie fulani, hakika shetani ana nguvu kubwa ya kumuangamiza binadamu.
If you don't know your self worth, basi ufahamu wako ndo utaona ni sawa tu kujitamba kwamba wewe ni men's incubator
 
Back
Top Bottom