BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 4,921
- 10,718
Ukisikia kuyabananga, basi mie komwe sio tu nimeyabananga, nimeyavaa jumla jumla. Nimeboronga, nimekanyaga divi bichi.
Baba mkwe wangu ni mwanajeshi, ana nyota nyingi begani, jitu jeusi, refu, linatisha na lina matuta usoni kama Mizengo Pinda.
Alikuja nyumbani kwangu kwenye sherehe ya kipaimara ya mjukuu wake. Kwa kweli amejua kufukia msosi, kaaah!! Amebugia mawali mpaka nikakimbia chumbani kujificha kwa muda nikawa namchungulia kwenye pazia!
Alipomaliza kula, akatuaga akaondoka. Baada ya masaa kadhaa, nikamuandikia ujumbe kumjulia hali yake ya safari!! LA HAULAAAH! Najutraaa!
Meseji ilipoenda, nikaona anapiga simu na kukata, nikajiuliza, Baba mkwe weraaah ayuuu!
Nikafungua meseji niliyomtumia kuhakikisha kama imefika, tobaaa weeee!!! Kumbe nimeandika madudu matupu, sijui nilikuwa nimelewa soda ya kipaimara komwe miee!
Meseji niliyoituma inasema "Baba Mkwe umefiRa salama?", badala ya Baba Mkwe UmefiKa salama?
Nimeizima simu ghafla, nikachukua panado nikameza, nikapiga goti nikasali rozari takatifu!
Naombeni mnifariji, sijui nifanye nini hapa! Msaada tafadhali, nimeyavaa, nimeyabananga!
Komwe limenishuka shuuuuu!