Nimemtongoza Mara mbili

Nimemtongoza Mara mbili

NduliCCM

Member
Joined
Jun 21, 2013
Posts
20
Reaction score
4
Wakuu heshima mbele.

Kuna msichana nilikutana nae mjini, nikampenda, nikamtongoza na akanipa namba ya simu.
Nilichat nae mara mbili tatu ivi na baada ya kuona haonyeshi kunipenda, nikampotezea, japo pia majukumu ya kazi yalinifanya nimsahau kwa muda.

Ikapita miezi michache, nikaja kukutana nae tena mjini, bila ya kumjua, nilimtongoza, ila yeye alikumbuka nilishawahi kumtongoza. Alinipa namba ya simu, nakatika kuingiza, jina lika-display.

Kiukweli huyu msichana sikumkumbuka kabisa, baadae nilikuja kumkumbuka. Nikaendelea kuchati nae.

Tatizo huyo msichana haniamini kabisa na amesema hatakuja kuniamini, anajua mi ni malaya ka Feruz kwenye ule wimbo wa Starehe.

Naombeni maujanja yenu nifanyaje ajue mi sio malaya? Mi nampenda kiukweli.
 
NduliCCM, Unaweza usipende kuambiwa ni malaya (if a man anaweza itwa hivyo pia sina hakika) BUT historia hii ambayo umeeleza inadhihirisha ni kwa namna ipi unachukulia suala la kutongoza kwa wepesi. Ni wazi kua unapotongoza mara nyingi husukumwa na sababu ya kutaka kulala nae ziaid kuliko kuwa nae na umtongozae akionyesha tu challenges hata kidogo huyoo unakimbia. Kitendo cha wewe kumtongoza miezi michache iliyopita kama ulivyokiri then ukamsahau - Ni picha ambayo kwa kweli haipendezi.

Ingekua kweli ulikua unampenda ungetafuta namna yingine ya winning her heart. Mtu ambae unapenda KWELI unatafuta kila namna kuhakikisha anatambua depth ya penzi lako hadi pale utakapojitahidi na mwenzio kuonyesha wazi kutojali hilo penzi lako.

Samahani... Hadi sasa nilipokusoma naungana na huyo dada, siamini kua kweli wampenda. Pengine kilichokusukuma wewe kutaka kumpata sasa ni kutambua kua hii ni mara yako ya pili kutongoza na dada kakulipia so somewhere inside of you unataka kujisafisha hiyo realisation kuliko hata vile ambavyo unataka kuwa nae.

Huu ni mtazamo wangu katika hili.
 
AshaDii mtazamo huo ndo na yeye anao. Kiukweli sio ivo mnavyomaanisha. Sasa kuna kitu gani nifanye nijisafishe?
 
Last edited by a moderator:
achana nae huyo bwana....wee kila leo kwenye relationship itakuwa ku-prove kjwa sio mgegedaji. sii utumwa huo.
 
AshaDii mtazamo huo ndo na yeye anao. Kiukweli sio ivo mnavyomaanisha. Sasa kuna kitu gani nifanye nijisafishe?


Nduli, hili ni kosa ambalo watu wengi huwa tunafanya... Huwa tunataka kutatua matatizo yetu ya kimahusiano kwa kuwahusisha wale ambao hawatutambui wala kuelewa kina cha mahusiano yetu.

Hili swali unauliza ni la msingi sana. Yapaswa umuulize huyo dada, kuwa sawa wakubali kuwa yeye ana mtazamo huo na unamwelewa kabisa; akupe yeye maelezo anataka wewe ufanye nini ili kuhakikisha kuwa unamaanisha unaposema unampenda.

Huu ushauri unaomba natamani huyo dada ndie angeomba, naamini nina mengi ya kumwambia upande wake kuliko upande wako. Ila sababu wewe ndie mwenye shida kwa sasa nakushauri mwambie (na amua iwe hivyo); kua umeamua humtongozi tena sababu hakuamini na "Trust" ni muhimu sana katika mahusiano. Mwambie kua unampenda na hotopenda kumpoteza hivyo kama atakubali basi wamuomba awe rafiki (wa kawaida na si wapenzi). Akikataa usilazimishe - believe me you ukimwambia hivo hata akikataa, atakutafuta tu kukusalimu na ndio itakua bora sababu mambo yataenda with flow.

It may take time... BUT kama kweli wampenda kama ulivyodai, eventually tu atakuwa rafiki yako kwa namna unataka wewe. Na akiwa rafiki yako zingatia haya;


  1. Be understanding.
  2. Be there for her.
  3. Usionyeshe desperation kana kwamba bado una hope ya kuwa nae kama mpenzi.
  4. Kua natural and be a genuine friend to her.

Sina guarantee kua it may work but you have to start from somewhere.
 
ahaahaha inaonekana hata hivyo kwamba akili yako ni ndogo kama ingekua ni memory kadi basi sijui ni mega ngapi maana unaonekana unasahau mapema mno
 
Lol. Kwa siku unatongozaga wanawake wangapi? Hauko smart hata kidogo!
 
ahaahaha inaonekana hata hivyo kwamba akili yako ni ndogo kama ingekua ni memory kadi basi sijui ni mega ngapi maana unaonekana unasahau mapema mno

Mkuu siunajua wanawake hawa, wakipendeza kidogo tu au akivaa wigi au kuvua anabadilika.
 
Huenda usiwe malaya, lakini kitendo cha kumtongoza mwanamke mara mbili pasipo kutambua hilo ni tatizo...

Mtu uliyempenda kwa dhati mara nyingi picha zao huwa hazifutiki akilini hata kama mawazo na hisia juu yake itafutika...

Ni kama tu unapoona kiatu au nguo ya mtindo fulani dukani na kushindwa kuinunua...nina amini siku nyingine ni lazima utaikumbuka na kama uwezo upo utainunua...
 
ahaahaha inaonekana hata hivyo kwamba akili yako ni ndogo kama ingekua ni memory kadi basi sijui ni mega ngapi maana unaonekana unasahau mapema mno

Hahahahaha, kweli JF inafurahisha
 
Umenikumbusha lecture wangu mmoja alikuaga na tabia kama yako sema yeye ilikua inaenda mbali zaidi maana atachunwa hadi hela na anatoa then akiachwa solemba hajali lakini cha ajabu baada ya miezi 3 akigongana na yuleyule mwanafunzi alomwacha solemba anaanza upya kumtongoza bila kujua ni repetition

Wanaume kama nyie naweza sema hamtongozi bali mnabahatisha na atakaenasa ndio huyohuyo, pia katika suala zima la kuaproach hua hamna vigezo vya msingi(factors) vinavyowasukuma kwa yule unaemtaka ndio maana unamwona-unamwaproach-hajarespond ulivyotaka-unampotezea on the spot............nijuavyo mimi once you you get across with something potential you wont get tired on one more try hata uwe busy vipi
 
Hahahaha yaani na hii id ya kuonyesha wewe ni mwanaccm inabidi uanze project mpya. Khadija Kopa kafiwa na mume majuzi, ungemchangamkia kumtoa msiba mbona ungeula!
Nyie wanawake inakuaje? yani ka mnaambiana majibu ya kuwajibu wanaume.
 
Hahahaha yaani na hii id ya kuonyesha wewe ni mwanaccm inabidi uanze project mpya. Khadija Kopa kafiwa na mume majuzi, ungemchangamkia kumtoa msiba mbona ungeula!

Mi sio mwanaccm. Hata Idd Amini aliitwaga nduli. unajua maana yake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom