Nimemtongoza Mara mbili

Nimemtongoza Mara mbili

Mkuu swala langu sio kutopenda kuitwa malaya (japo sio malaya), swala ni jinsi gani nitarudisha imani kwa huyu msichana, anaipende ka mi nnavyompenda.

time will tell,endeleeni taratibu you will build that trust

ila hata mimi if I was her ningekufikiria the same tu
 
Mkuu swala langu sio kutopenda kuitwa malaya (japo sio malaya), swala ni jinsi gani nitarudisha imani kwa huyu msichana, anaipende ka mi nnavyompenda.

Kinachowashangaza wengi ni kuwa imekuwaje umsahau huyo binti wakati ulikuwa unampenda, maana kitendo hiki hakitofautiana sana na kumsahahu mchumba au mke wako kabisa.
 
Kinachowashangaza wengi ni kuwa imekuwaje umsahau huyo binti wakati ulikuwa unampenda, maana kitendo hiki hakitofautiana sana na kumsahahu mchumba au mke wako kabisa.

Nilionana nae mara mbili tu. Yani wakati namtongoza mara ya pili, ilikua siku yangu ya pili kuonana nae baada ya kutokuwasiliana nae kwa miezi kadhaa.
 
NduliCCM, Unaweza usipende kuambiwa ni malaya (if a man anaweza itwa hivyo pia sina hakika) BUT historia hii ambayo umeeleza inadhihirisha ni kwa namna ipi unachukulia suala la kutongoza kwa wepesi. Ni wazi kua unapotongoza mara nyingi husukumwa na sababu ya kutaka kulala nae ziaid kuliko kuwa nae na umtongozae akionyesha tu challenges hata kidogo huyoo unakimbia. Kitendo cha wewe kumtongoza miezi michache iliyopita kama ulivyokiri then ukamsahau - Ni picha ambayo kwa kweli haipendezi.

Ingekua kweli ulikua unampenda ungetafuta namna yingine ya winning her heart. Mtu ambae unapenda KWELI unatafuta kila namna kuhakikisha anatambua depth ya penzi lako hadi pale utakapojitahidi na mwenzio kuonyesha wazi kutojali hilo penzi lako.

Samahani... Hadi sasa nilipokusoma naungana na huyo dada, siamini kua kweli wampenda. Pengine kilichokusukuma wewe kutaka kumpata sasa ni kutambua kua hii ni mara yako ya pili kutongoza na dada kakulipia so somewhere inside of you unataka kujisafisha hiyo realisation kuliko hata vile ambavyo unataka kuwa nae.

Huu ni mtazamo wangu katika hili.

Mkuu chukua tano! Umeongea point sana, kama dogo anazo kichwan atajiongeza.
 
Nilionana nae mara mbili tu. Yani wakati namtongoza mara ya pili, ilikua siku yangu ya pili kuonana nae baada ya kutokuwasiliana nae kwa miezi kadhaa.

Kweli haupo kwake ila unajifanyiza....fikiri msichana umempenda na namba ya simu kakupa then umekaa huko hata hukuwahi kumjulia hali leo unakuja na kumtongoza tena na anakupa namba tena japo alikufahamu.....hapa tayari inaonyesha wewe hujatulia na ulimtaka kimapenzi na siyo kumpenda kama usemavyo na ndio maana hakuwa moyoni mwako. Wanaojua kupenda jamaa yangu msichana akishaingia moyoni maisha yako yote utaikumbuka sura yake. Binafsi kuna msichana nilimpenda ila tukatengana kabla sijaeleza hisia za moyo wangu ila ni miaka 12 imepita sura yake bado naikumbuka kama nimemwona jana. Ushauri kama unampenda kwa dhati fuata ushauri wa my dada AshaDii hapo juu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom