Nimemsikia Waziri akisema Hivi...........

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Leo siku ya Jumamosi 28/6 muda kama wa saa 5.30, nilimsikia Waziri wa
Fedha Mh. Sada Mkuya aki wind up mswada wa sheria ya fedha akisema kwa kiingereza: 'I
can see a huge different.....'

Huu mtindo wa wabunge kuchanganya kiingereza na kiswahili bungeni ninaupinga sana.
Waziri huyu kaacha kutumia kiswahili akatumia kiingereza ambacho si sahihi.Kwa nini mnapenda
kung'ang'ania lugha ngeni na kuacha lugha yetu nzuri ya kiswahili? Na
mnapotumia hicho kiingereza mnakosea vibaya sana!
Ninachojiuliza: Je, mtu hawezi kufahamu kiwango cha ufahamu wake wa lugha fulani?
Na ukifahamu kwamba uwezo wako wa kiingereza ni mdogo, huwezi kwenda English course?

Mimi kwa mawazo yangu kuna wabunge na mawaziri wanahitaji kozi kali ya business english.
 
Ogopa sana kujiweka katika nafasi fulani ya juu ingawa ki-uhalisia ni tupo chini saaana......tunang'ang'ania kiingereza na huku kiswahili ni patashika nguo kuchani...yaaani full-kupoteana
 
Tatizo malimbukeni weng hudhani wakitupia vineno vya kiingereza ndo wataonekana wasomi kumbe mambu-bu na hata position walizopewa n kiswaiba au ki jk zaidi.
 
Hapo ukimuambia aongee english frequent maneno yatakayo sikika common ni the the the the
 
Umesema umesikia
Inawezekana umesikia vibaya
Mizizi, usitumie ufahamu wako wa mantiki ya maneno ya kiswahili kunivuruga. 'nimemsikia' nimemsikiliza' kwangu yote yana maana moja.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom