Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,727
Siku za karibuni nimesafiri na Prof. Kabudi kwenda Nairobi. Tuliongea mengi na ninaamini atazingatia.
Lakini moja ya tuliyoongea naye na nikalazimika kukubaliana naye ni juu ya nafasi ya Tundu Lissu katika siasa za Tanzania. Mimi nilikuwa na maoni kinzani na yeye alikuwa anaona fahari sana juu ya kazi anayofanya Tundu Lissu. Kwa kauli yake aliniambia, " Tundu hana mtu wa kumjibu ndani ya serikali na hatapatikana karibuni".
Nimeangalia hotuba yake Prof. Kabudi kwa mshangao pale alipokuwa akimshambulia Tundu baada ya kuwa amenishawishi nimkubali Tundu. Je yawezekana Prof. Kabudi anaelekea kuangukia mtego alimoangukia Prof. Muhogo ambaye aliingia kwa kishindo akitanguliza uprofesa lakini akajikuta anaangukia mikononi mwa wakulima na wavuvi wa Musoma na kuwapigia magoti na kula udaga nao ili wampe kura. Siku hizi amenywea.
Baba wa Taifa ambaye ni role model wa Prof. Kabudi, aliandika akishauri kuwa " wana falsafa wanajua kutawala lakini hawapendi kutawala". Akasema, kila walipopata nafasi ya kutawala, walipenda wamalize haraka na kurudi katika kazi yao wanayoipenda.
Awamu hii ina maprofesa wengi. Nachelea watadhalilishwa wasipokuwa waangalifu.