Je, kuna tofauti yoyote kati ya taarifa aliyotoa Lissu na aliyotoa Prof. Kabudi kuhusu kukamatwa kwa ndege nchini Canada?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,756
Flashback: August, 2017

Hapo juu Mh. Tundu Antiphas Lissu, aliyekuwa Mbunge wa kuchaguliwa na mwakilishi wa wananchi wa Singida akitoa taarifa ya kukamatwa kwa ndege yetu nchini Canada.

Fast-forward: November, 2019

Hapo juu Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa kuteuliwa wa Mambo ya nje akitoa taarifa ya kukamatwa kwa ndege yetu tena nchini Canada.

Takafuri...

Mh. Tundu Antiphas Lissu baada ya kutoa taarifa hii muhimu kwa wananchi wa Tanzania alituhumiwa kutumiwa na mabeberu na kuitwa msaliti.

Prof. Palamagamba Kabudi baada ya kutoa taarifa kama hiyo hiyo aliyoitoa Mh. Tundu Antiphas Lissu amepongezwa na kusifiwa kwa uzalendo.

Ndugu zangu Watanzania, je kuna lolote tunajifunza hapa? Naomba maoni yenu yasiyo na jazba wala kebehi. Tanzania ni yetu sote na sidhani kama yuko Mtanzania asiyelitakia mema taifa letu.
 
Kila nikiandika komenti nafuta. Nakushauri tuendelee kupumzika ndugu yangu.
Andika tu ndugu yangu, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya akisema, "Mfichaficha maradhi, kilio humuumbua." Wahenga nao walisema, "Dawa ya deni ni kulipa." Wafilosophia nao walisema, "Historia nayo ina tabia moja, hujirudia."

Historia inatakiwa iwe Mwalimu, Tabibu na Mtabiri. Kosa si kosa ila kurudia kosa. Once bitten twice shy!
 
Na bado subiri wachina waanze kudai madeni yao, tutauza ikulu iwe ya Chamwino au Magogoni.
 
IMG_20191123_111638.jpeg
IMG_20191123_111642.jpeg
 
Natamani kila moja amsikilize kwa umakini mkubwa anayoongea Mh. Tundu Antiphas Lissu halafu ajiulize, je nia ya Mtanzania yeyote yule kutaka kumdhuru ilitokana na nini?
WanaumbukaAa..
 
Kuna tofauti kubwa. Mmoja kaitoa kwa kufurahia kitendo kile na mwingine kwa kusikitikia kitendo kile. Wewe pia umeitoa kwa kupongeza kitendo cha kukamatwa hiyo ndege. Kushangilia kukamatwa hiyo ndege na nyingine ni uhaini
 
Hujasikiliza kwa makini anachoongea Mh. Tundu Antiphas Lissu, hashangilii, la hasha, anaongea kwa uchungu sana akisikitika na kuonya yanayoweza kutupata mbele ya safari kama hatukuchukua hatua stahiki..
 
Back
Top Bottom