Nimemshauri Kabudi amuulize Prof. Muhongo

Siku za karibuni nimesafiri na Prof. Kabudi kwenda Nairobi. Tuliongea mengi na ninaamini atazingatia ...

Nimeangalia hotuba yake Prof. Kabudi kwa mshangao pale alipokuwa akimshambulia Tundu baada ya kuwa amenishawishi nimkubali Tundu. ...

Awamu hii ina maprofesa wengi. Nachelea watadhalilishwa wasipokuwa waangalifu.

Bandiko lako lina mantiki kiasi.

Ni kweli Maprofesa kiutawala kwa masuala ya kijamii hushindwa kwa sababu maono yao yanakuwa mbali sana na wanaowaongoza.

Ushahidi ni pale bungeni Prof Kabudi alipolibadirisha bunge kuwa darasa lake la sheria. Hivyo si sahihi kusema kwamba alikuwa anamshambulia Mh Lissu ila alikuwa anamkumbusha maadili ya mwanasheria ya kutumia maneno yenye staha. Akamtolea mfano wa mwingereza, mwenye maadili bungeni, hamwambii mwenzake "stupid". Lakini Mh. Lissu hutumia maneno makavu kama kijana wa kijiweni, katika kujenga hoja zake.

Nadhani itafaa Maprofesa wakatumiwa kama washauri wa Serikali kuliko kuwapa madaraka ya Uwaziri.
 
Duh! Mara nyingi mwanafunzi kwa utundu wake anaweza kabisa kuwa mahiri kuliko mwalimu wake. Bado sijaona point ya maana kutoka kwa wa kubagazana yenye umahiri zaidi ya Kamanda Lissu zaidi ya kufoka, kukunja uso na kutoa macho wakati akiongea ili hali kama Waziri wa Sheria yuko kimya kuhusu vyeti fake vya mhuni na jambazi Bashite na uvamizi wake yuko kimya kuhusu PROPESA Lipumba na uhuni anaoufanya dhidi ya CUF halali na pia uvamizi wa kuwapiga CUF halali na waandishi wa habari.

Shida kubwa iliyopo ni Prof Kabudi kum-outshine Lissu. Hili limewakera na litaendelea kuwakera wengi na kupelekea mashambulizi mengi yenye lengo la Personality assassination kwa Prof Kabudi.

Kuna watu katika jamii hii wanaona ni kosa la jinai kwa mtu kutoka upande wa serikali au chama tawala kuwa mweledi. Siasa hizi hazituletei tija sana!
 
Hv Mshahala Wa Mhadhiri Unaweza Kua Kiasi Gan Kwamfano Hasa Kwa Wale Wa Muda Mrefu Km Yeye? Labda Tungeanzia Hapo. Lait Km Madaktar Bingwa Na Wasomi Nguli Ktk Vyuo Vyetu Wangekua Wanalipwa Vzr, Cdhan Km Wangekua Wanakubali Apointment Km Hzo Za Kudhalilishana. Me Cjasoma Sheria Lkn Nkajikuta Nacheka Baada Ya Kuckiliza Point Zake. Hv Duniani Nchi Zilizo Na Katiba Ni Ngapi, Na Ziczo Na Katiba Ni Ngapi? Kwa Nn Asingefkria Zenye Katiba Akakmbilia Zczokua Nayo? Kwann Actolee Mfano Nchi Zilizo Afrika? Kaz Kwel Kwel, Kuna Yule Mama Tibaijuka, Yule Ndo Balaa. Nlimuona Pale Nkuruma Kwenye Mdahalo, Ni Shida Hata Kujieleza Tu Majanga, Anachangia Point Zenyewe Pumba Tu. Usipo Soma Shida, Pia Ukisoma Shida.
Hii lugha uliyoandika ni kiyunani au kiajemi ....
 
======
Unakosea sana. Prof. Kabudi ni Profesa wa sheria. Outshinning Tundu is the obvious case.
Hata Tundu hana shida na hilo.
Shida kubwa ni mabadiliko ya ghafla ya Profesa Kabudi. Juzi alikuwa anamkubali Tundu; jana akaonekana anamshambulia. Mwaka jana alikuwa anatetea serikali tatu, jana anatetea serikali mbili na kuzitumikia.
Hata alipoitwa kama 'friend of the Judiciary' katika kesi ya mgombea binafsi katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania iliyofunguliwa na marehemu Mch. Mtikila (RIP), alionyesha udhaifu mkubwa kwa kuegemea kwenye matakwa ya serikali badala ya uhalisia wa haki za watu katika kuchagua na kuchaguliwa.
Hana tofauti na wachumia tumbo wengine, na naamini hivi karibuni atayakana hata machapisho yake.
 
ungekua walau umewahi kukanyaga ardhi ya chuo kikuu ungejua kuwa Tanzania tuna maprofesa.
hapo umeniquote Kama mtu asiyejiamini... Elimu ni kuelimika na sio kufaulu... Unaposema kufika kwenye ardhi ya chuo kikuu wengi wamefika na kukamyaga... Ungekuwa mwerevu mtu ulie smart Hoja yako ingekaa sawa sawia. Kuwa profesa ni kutunukiwa shahada na hiyo Sshahada huwezi kutembea nayo Kama kitambulisho... Hata hapo chuoni hawatembei nazo.

Kwa Tanzania hii ukiambiwa huyu Fulani ni profesa na ukimfuatilia ni mauozo tu anatema so wangeachwa huko huko vyuoni kuliko kujiaibisha hadharani kwa vituko..
Ndio Yale ya kina Isaac Newton wanasahau Kama walikula chakula n.k hawafai kuongoza nchi. Tumewaona siku nyingi kina kapuya n.k yaani ni mauharo tu. Chaki zinawafaa
 
Ina maana mkuu huyo Pro Kabudi ni Kinyonga anabadirika kutegema yupo wapi.
Ana sura zaidi ya mmoja,na anaweza akatetea hoja yake kutegemea yupo wapi.Walakini hiyo inamtofautisha na mawakili kama Marehemu Madiba Mandela na sasa tunaye wakwetu Lissu wako tiyari kusimamia ukweli hata kama watafungwa jela.
Viva Lissu.
Ni afadhali kinyonga, ongezea yule mdudu anayefanana na nyoka akienda pande zote bila kugeuza kichwa, maana pande zake zote ni kama kichwa. Anapenda kufuatana na siafu pindi wanapohamia makao mapya.
 
kabudi ajue kuwa pale mjengoni sio nkrumah hall!pale atazomewa hata na sugu au majimarefu,kibajaj au kilaza yeyote na hakuna cha kumfanya.kama spika kaitwa fal....a yeye ataitwaje na uzee ule,shauri yake
 
======
Unakosea sana. Prof. Kabudi ni Profesa wa sheria. Outshinning Tundu is the obvious case.
Hata Tundu hana shida na hilo.
Shida kubwa ni mabadiliko ya ghafla ya Profesa Kabudi. Juzi alikuwa anamkubali Tundu; jana akaonekana anamshambulia. Mwaka jana alikuwa anatetea serikali tatu, jana anatetea serikali mbili na kuzitumikia.
wewe unageuza kama kamgeuka but in fact wanafundishana.. ni vita ya kisomi ndio maana Lisu muda wote alikuwa anacheka na kupiga meza... Sio kamgeuka ila amepata nafasi ya kumwonyesha mwenzake anachokijua kisomi.
Ni suala la academic na sio kumpinga ama kutofautiana nae.,. naamini bado anamkubali na watabaki good friends ila wewe ndio unashida ya kutoelewa kuwa kumkubali mtu sio kumshikia kanzu ama kutopingana ama kuongea neno linalofanana.
Again I dont see kumpinga ila ni kujengana kwa hoja
 
Prof Kabudi anashambuliwa sasa kwa sababu ameonekana ni tishio kwa Lissu, uzuri bajeti ya wizara yake imeshapita, ila ni wazi Lissu alikuwa kama darasani juzi bungeni.
 
======
Unakosea sana. Prof. Kabudi ni Profesa wa sheria. Outshinning Tundu is the obvious case.
Hata Tundu hana shida na hilo.
Shida kubwa ni mabadiliko ya ghafla ya Profesa Kabudi. Juzi alikuwa anamkubali Tundu; jana akaonekana anamshambulia. Mwaka jana alikuwa anatetea serikali tatu, jana anatetea serikali mbili na kuzitumikia.
Sijajua,kwa fani zingine,lakini kuna fani zingine kama za Uhandisi,Prof anaweza akawa mjuzi wa theory sana lakini mwanafunzi wa shahada ya kwanza au ya pili akawa yuko vizuri kwenye kazi,siyo makaratasi. Naamini pamoja na Umahiri wa Prof Kabudi,lakin anajua kabisa msomi wa Sheria Tundu Lissu siyo mtu mwepesi,ni mtu mwenye shahada ya Pili kutoka Uingereza. Pamoja siyo profesa lakini ana madini mengi kichwani. Ukitaka kumzidi kwa hoja lazima ujipange.

Kuhusu darsa la jana pale Bungeni ni jambo jema,ila mengi yaliyozungumzwa najua wengi wa wanasheria watakua walikua wanayafaham.
 
Siku za karibuni nimesafiri na Prof. Kabudi kwenda Nairobi. Tuliongea mengi na ninaamini atazingatia.

Lakini moja ya tuliyoongea naye na nikalazimika kukubaliana naye ni juu ya nafasi ya Tundu Lissu katika siasa za Tanzania. Mimi nilikuwa na maoni kinzani na yeye alikuwa anaona fahari sana juu ya kazi anayofanya Tundu Lissu. Kwa kauli yake aliniambia, " Tundu hana mtu wa kumjibu ndani ya serikali na hatapatikana karibuni".

Nimeangalia hotuba yake Prof. Kabudi kwa mshangao pale alipokuwa akimshambulia Tundu baada ya kuwa amenishawishi nimkubali Tundu. Je yawezekana Prof. Kabudi anaelekea kuangukia mtego alimoangukia Prof. Muhogo ambaye aliingia kwa kishindo akitanguliza uprofesa lakini akajikuta anaangukia mikononi mwa wakulima na wavuvi wa Musoma na kuwapigia magoti na kula udaga nao ili wampe kura. Siku hizi amenywea.

Baba wa Taifa ambaye ni role model wa Prof. Kabudi, aliandika akishauri kuwa " wana falsafa wanajua kutawala lakini hawapendi kutawala". Akasema, kila walipopata nafasi ya kutawala, walipenda wamalize haraka na kurudi katika kazi yao wanayoipenda.

Awamu hii ina maprofesa wengi. Nachelea watadhalilishwa wasipokuwa waangalifu.

mkuu wana jidhalilisha wenyewe na hali hiyo inatufanya tuamini kumbe u profesa sio lolote wala chochote, kama hali ya maisha inazidi kua ngumu na wameshindwa kukuza uchumi huku biashara zikifa na bashite akishindwa kushughulikiwa sioni umuhimu wa elimu zao zaidi ya majigambo tu na kula kodi zetu.
watadhalilika saana huu ni mwanzo tu.
 
Shida kubwa iliyopo ni Prof Kabudi kum-outshine Lissu. Hili limewakera na litaendelea kuwakera wengi na kupelekea mashambulizi mengi yenye lengo la Personality assassination kwa Prof Kabudi.

Kuna watu katika jamii hii wanaona ni kosa la jinai kwa mtu kutoka upande wa serikali au chama tawala kuwa mweledi. Siasa hizi hazituletei tija sana!
Ukitaka kumkamata kuku kirahisi mtupie mahindi huku ukielekea ndani.. That's it
 
Tundu Kwa sasa anatia huruma sana, huku Tulia, kule Palamagamba patamu, misifa yote kwishiney
Mkuu mtu anapokuwa na mpinzani hujipanga sana ilikujikwamua pale alipo, hawa watamfanya Lisu kuwa bora zaidi kwani hata bweteka
 
======
Unakosea sana. Prof. Kabudi ni Profesa wa sheria. Outshinning Tundu is the obvious case.
Hata Tundu hana shida na hilo.
Shida kubwa ni mabadiliko ya ghafla ya Profesa Kabudi. Juzi alikuwa anamkubali Tundu; jana akaonekana anamshambulia. Mwaka jana alikuwa anatetea serikali tatu, jana anatetea serikali mbili na kuzitumikia.
HAPO SASA...
 
Back
Top Bottom