Danisamweswa
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 453
- 154
Naombeni kujua kosa langu ni nini? Ilikuwa siku ya birthday ya mpenzi wangu. Ninavyomjua huwa anapenda sana kulala. Basi mojawapo mwa zawadi nilizomnunulia ni mto (Pillow). Nilimwambia wazi kuwa nimekununulia pillow kwa kuwa ninajua unapenda sana kulala. Duh! kumwambia hivyo akachukia na wala zawadi hiyo hakuipokea. Naombeni kujua kama nilikosea au la. Binafsi sijaona kosa langu kwani nilikuwa na nia njema tu kumpa zawadi hiyo.