umemkosea heshima.hebu fikilia wewe boss wako akunyang'anye simu utajiskiaje.kama umemchoka mrudishe kwao kuliko kumnyanyasa kwa vitu vodogo vidogo.kwani nyie ndo mtamuoa?.au hamtaki awe na malafiki.kwani yeye mfungwa?.acheni ukilitimba.mia
Hongera kwa kutambua mabaya ambayo anayafanya beki tatu wako,kuna mambo yananitatiza kidogo na naomba uniweke sawa.
1.Wakati unanchukua huyo beki tatu ulikuwa unajua kuwa ni mtu mzima na atakuwa anahitaji haki zake za msingi za kuwa na mahusiano?
2.Ulipokuwa unamnunulia simu au kukubali awe na mawasiliano ulitaka awe anawasiliana na nani?
3.Je siku hizi ukiwa na tatizo au nyumba yako ikiwa imevamiwa au kuugua ni nani atakupa taarifa?
4.Ulishindwa nini kumwambia kuwa pale kwako hutaki waje wavulana na kumwachia simu?
Ni hayo tu mkuu.
mmh! sijapenda,!! unajua mkuu na yy ni mwanadamu kama walivyo wengine,umemnyanganya cm lakini si gengeni anaenda basi jiandae kupata shemeji muuza genge!! mkalishe chini sema nae taratibu MRUDISHIE SIMU YAKEEEEEE!! ALLAA!!
yuko kwa age ya 25yrs
sikubaliani na kitendo cha housegirl kuleta vivulana vyake nyumbani kwako, atakuharibia watoto, nakumbuka wakati nikiwa mdogo housegirl alikua anatufungia balcon yeye anajirusha ndani, kama hatujala mchana huo imekula kwetu!! tukianguka tukaumia imekula kwetu, ila nashukuru sikujua wakitufungia huko wao ndani wanafanya nini la sivyo mmmmmh.
lakini pamoja na yote hayo mrudishie huyo binti simu yake, asije zidiwa mihemko akamwinda baba watoto wako. lakini kabla hujamrudishia ni vyema ukazungumza nae umwambie ukweli hutaki vivulana vyake hapo, na ukimfuma nao tena hiyo ajira ndo bye bye, mweleza madhara ya mapenzi bila kinga na ajue akinasa hana lake hapo, maana kama ana umri wa miaka 25 huyo ni mtu mzima kama ana akili atashika maneno yako, meanwhile uwe unarudi home mara kwa mara mida tofauti msuprise ucheki anafanya nini.
Simu ni kwa ajili ya mawasiliano ya kujenga na sio kubomoa. Au unadhani kwa kuwa Mungu amekupa hicho kinaniii chako basi ndo ukitumie tu hovyohovyo hata kwa matumizi yasiyo na maadili? Au tuseme ukimuweka mlinzi akulindie mali zako basi ni ruhusa yeye kukuibia?
poleee, huwa ni ujana tu unawasumbua wengi wao, especially kama ulimtoa bush huko kaja kujanjarukia towan... rudisha kwao mpe chake, tafuta mwingine (tena ikiwezekana muwe related japo kidogo) , ataona haya kufanya mambo ya ajabu ajabu at your place. cha msingi shukuru Mola hao viboy (sijui nao ni age mate wake au anasalandiwa na viserengeti) hawajafanya shambulio hapo kwako, either wizi au hata kumrubuni kukuibia au kuwamolest watoto wako.