Safina Bahari
Member
- Apr 5, 2020
- 38
- 42
Idadi sahihi ya matundu ya neti ni IPI..
Mm huwa anani expires Sana huyu jamaaUnani insipaya sana sio siri
we ni kichaaRafiki yangu wa damu tangu tukiwa watoto hadi utu uzima naomba niwie radhi sana.
Leo nimeona niwape kisa ambacho kilipelekea urafiki wangu na yeye kufika tamati. Siku moja nilikuwa nyumbani nimefua nguo zangu na matandiko nikaweka safi majira ya mchana nguo zilikuwa zimekauka nikaanza kukunja na kurudishia neti ambayo nilifua pia.
Baada ya kukunja nguo na kutandika vizuri kitanda nilikaa bila kazi mle ndani. Ghafla wazo likaniijia kwa nini usihesabu matundu ya neti uone yako mangapi. Kweli nikaona ni kitu kizuri kwa kuwa mimi ni mdadisi sana nikikaa sehemu lazima nidadisi vitu. Basi nikaanza kuhesabu yale matundu taratibu mara mlango ukagongwa, sikuitikia maana nilikuwa natakiwa niwe makini sana kuhesabu yale matundu.
Mlango ukaendelea kugongwa kwa fujo nikaona mahesabu yataharibika nikaweka alama nilipoishia nikaenda kufungua mlango nakuta ni rafiki yangu kaja kunisalimia. Nikamkaribisha na kumwambia atulie asinichanganye wakati naendelea na mahesabu. Basi dakika kama 10 tuko kimya mle ndani niko bize na yangu na yeye ananitazama tu. Nikahesabu hadi tundu la 3560 akanishika bega na kuniuliza unafanya nini? Akaendelea kunishika bega na kunitikisa na nikapoteza hesabu ya yale matundu, nilishikwa na hasira nikaamka na kumpiga ngumi karibu na koromeo. Rafiki yangu nilisikia analalamika umeniua kwa nini.
Nilitoka nje na hasira sana, ikabidi niende kwao na kuwaambia waje nyumbani mtu wao kaanguka ndani kwangu. Wakaja na kumbeba kwenda hospitali alizinduka jioni sana. Baada ya kuzinduka akaniita na kuniuliza sababu ya mimi kumpiga vile hadi azirai, nilimwambia alinichanganya wakati nahesabu matundu ya neti, akauliza tena: kwahiyo matundu ya neti ni muhimu kuliko urafiki wetu? Sikuwa na jibu nikaomba anisamehe ila hakutaka tena msamaha na urafiki ukaisha toka siku ile.
Hadi leo rafiki yangu amenunua pikipiki huwa nakaa nasema kama bado tungekuwa ni marafiki ningekuwa naendesha ile pikipiki ila amekataa hata kunisamehe.
Namkumbuka sana rafiki yangu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ulichoandika kina ukweli aisee. Huyu jamaa ana imagination kubwa sana! Mtu wa kawaida huwezi ukafikiria vitu kama hivi! Jamaa anatakiwa kuelekeza huu uwezo wake kwenye mambo yenye manufaa.mtu mwenye IQ ndogo hawezi kuandika vitu kma unavoandika.. ndo mana tunasema there is a very thin line between geniousity and stupidity! ...
Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya yote ni nani anayeweza kuhesabu matundu ya net?
Jr[emoji769]
Yani mtu kuamua kuchekesha watu Ni bipolar...toka huko nakujifanya umesoma Sana.Una tatizo la akili,linaitwa acute bipolar disorder,kamuone daktari wa magonjwa ya akili
Kwaiyo wenye matatizo ya Akili wanapimwa kwa kuangalia sura...Wewe Ni bogus kabisa... kabombeAkkiona tu sura yako atajua tu kuwa una tatizo la akili
Wodi ya vichaa hakuna kupimana damu.wala haja kubwa
Naamini viwanda vya neti vitakua vinajua...tufanye researchIdadi sahihi ya matundu ya neti ni IPI..