Habari zenu humu ndani.
Mwenzenu leo sina furaha sana maana akili yangu yote inamuwaza Hajir mpenzi wangu tuliyeachana nae kama miezi zaidi ya minne sasa.
Sema ukweli nilikuwa nampenda sana Hajir wangu. Tangu tuachane nimejaribu kuingia kwenye mahusiano mapya kama mara tatu hivi lakini wapi, sipati furaha kama niliyokuwa nayo nilipokuwa na Hajir.
Nakumbuka tulipoachana nilifuta namba yake ili nikate mawasiliano naye kabisa. Hili halikusaidia maana namba take imo kichwani mwangu.
Anyway, kama yumo humu naomba anisamehe kwa niliyomtendea anisamehe tuishi kama zamani. Niliyokufanyia ilikuwa ni hasira tu Hajir mpenzi wangu. Nakupenda sana.
[/QUOT
Kifungu cha sheria za ubaharia namba 17 (a) na kifungu kidogo cha kanuni za maboresho ya sheria kuu za ubaharia namba 65 (b), (c), (d) na (e) vinatoa katazo kwa baharia kulilia mwanamke alietemana nae tena mbele ya mabaharia wenzake kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kujichimbia kaburi ww mwenyewe na kuwafanya wale mabaharia waliowahi kumtamani manzi yako sasa kumfuatilia kwa nguvu maana ushatoa taarifa kuwa hampo tena kwenye mahusiano.
Usikwame baharia!