Nimemkumbuka Andres Escobar

Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
5,482
7,459
Katika Fainali za Kombe la Dunia 1994, kikosi cha Colombia kikiwa na wachezaji mahiri kama akina Faustino Aspirilla, kilitolewa hatua za mwanzo bila matarajio ya wengi baada ya kufungwa 2-1 na Marekani kufuatia Goli la kujifunga la Andres Escobar.

Siku chache baadaye, Andres Escobar alipigwa risasi katika night club kwa kile kilichoelezwa mashabiki kutofurahishwa na kutolewa kwa timu yao ya Colombia kwa kupoteza mchezo dhidi ya Marekani kwa Goli la kujifunga la mchezaji huyo. Wengine wanadai ni wacheza kamali ambao waliliwa pesa zao kutokana na matokeo hayo.

Manojua vema hebu tukumbusheni tukio hili huenda likaongeza umakini kwa hawa watoto wa leo wanaoharibu "clean sheet" za watu bila mpango.

NB: mada haiuhusiani na mchezo wa leo.
 
dunia nzito sana kwa kweli, jamaa alikua yupo kwenye peak kabisa, alikua antegemea kusajiliwa Inter Milan au Ac Milan yupo kwenye mazungumzo mauti yalipomkuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom