Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,723
- Thread starter
- #81
Wanabodi,
Naomba kukiri kumfahamu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kitambo kidogo na kuwahi kukutana naye na kutambulishwa kwangu, kiukweli nilimuona ni mtu anayejisikia sana!, anajiona sana na anainga sana, ukijumlisha na zile kauli zake za utumbo utumbo enzi zile, kiukweli kabisa nilimuona ni mtu wa hovyo hovyo tuu hata apewe madaraka gani!. Hivyo alipoteuliwa kuwa DC wa Kinondoni, mengi aliyoyafanya niliyahesabu ni muendelezo wa kutafuta masifa tuu!.
Kwa maoni yangu, niliona nafasi za UDC ni wastage of time, money and resources, na ma DC zaidi ya kuwa wakuu wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya, ni watu wasio na lolote la maana la kufanya, lakini DC Makonda, ameupa u DC hadhi, Ma DC sasa wanaonekana ni watu wa maana, na DC wa Kinondoni anaimpact kuliko hata RC, hivyo position inayomstahiki ni kuwa RC wa DSM!.
Leo nimemsikia akizungumza katika tukio la Malkia wa Nguvu lililoushwa live na Clouds TV, kiukweli nimeguswa sana na aliyoyasema kuhusu bughudha kwa wafanyabiashaa ndogo ndogo kuzungushwa kuhusu vibali!.
Akamuagiza ofisa biashara wake kokote aliko, kama hakutazama TV, au kusikiliza redio kuhusu agizo hilo, then mke wake au watoto wake watakuwa wamesikia hivyo wampe ujumbe baba yao kuwa kuanzia Jumatatu, hakuna kukaa ofisini kubugudhi vafanyabishara, bali atoke nje kukagua biashara na kutoa leseni papo kwa papo, na yeye DC kwa upande wake, kuanzia Jumatatu, ataweka dawati maalum la wafanyabiashara watakao bughudhiwa au kuzungushwa zungushwa, waripoti kwake direct, halafu huyo ofisa anayewazungusha, ataipata habari yake!.
Kiukweli, watu wa aina ya DC Makonda, ndio wanaohitajika kukabidhiwa jiji kama la Darisalama, kiukweli jiji litanyooka!.
Natoa wito kwa Mhe. Rais Magufuli, kufuatia RC wa DSM, Said Meck Sadick kufikisha umi wa kustaafu kwa mujibu wa sheria, (just by look), tunakuomba ututeulie DC Makonda awe RC wa DSM, atakusaidia sanna wewe na serikali yako, kayika utekelezaji wa falsafa yako ya "HAPA KAZI TUU!".
Katika sherehe hiyo ya Malkia wa Nguvu, DC Makonda amedhihirisha wazi yeye ni Balkia wa Nguvu!.
Hongea Sana DC Makonda, sasa unastahili U RC-DSM!.
Naomba kuwasilisha.
Pasco
- Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
P.