Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,677
- 119,310
Wanabodi,
Naomba kukiri kumfahamu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, tangu kitambo kidogo kwa Paul kutambulishwa kwangu nikiwa mjini Dodoma, pale Dodoma Hotel, kiukweli nilimuona kama ni mtu anayejisikia fulani!, anajiona na kama anaringa fulani, ukijumlisha na zile kauli zake za utumbo utumbo za enzi zile kumhusu yule "jamaa yetu", kiukweli kabisa nilimuona ni mtu wa hovyo hovyo tuu na hana maana yoyote hata apewe madaraka gani!. Hivyo alipoteuliwa kuwa DC wa Kinondoni, kiukweli nilimpuuzia tuu na hivi vyeo vya kupeana kwa kuangaliana usoni!, mengi aliyoyafanya kwanza, niliyahesabu ni muendelezo wa kutafuta misifa tuu!.
Kwa maoni yangu kuhusu nafasi za UDC, nilikubaliana na maoni ya Tume ya Warioba, Ma DC ni muendelezo wa colonial legacy ambao kwa sasa ni wastage of time, money and resources, hivyo wako supposed kuwa redundant.
Ma DC zaidi ya kuwa wakuu wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya, ni watu wasio na kazi nyingine yoyote au lolote la maana la kufanya, lakini kiukweli kabisa, huyu DC Makonda, umeuheshimisha sana UDC, ameupa hadhi na heshima ya pekee ya ziada u DC, Ma DC sasa wanaonekana ni watu wa maana!, kupitia U DC wa Kinondoni, Paul Makonda emeleta impact kuliko hata RC wa DSM, hivyo position inayomstahiki huyu DC wa Kinondoni wa sasa, bwana Paul Makonda, ni kuwa RC wa DSM!.
Leo nimemsikia akizungumza katika tukio la Malkia wa Nguvu lililorushwa live na Clouds TV, kiukweli nimeguswa sana na aliyoyasema kuhusu bugudha kwa wafanyabiashara ndogo ndogo kuzungushwa kuhusu vibali!.
Akamuagiza ofisa biashara wake kokote aliko, kama hakutazama TV, au kusikiliza redio kuhusu agizo hilo, then mke wake au watoto wake watakuwa wamesikia hivyo wampe ujumbe baba yao kuwa kuanzia Jumatatu, hakuna kukaa ofisini kubugudhi wafanyabishara, bali atoke nje kukagua biashara na kutoa leseni papo kwa papo!, na yeye DC kwa upande wake, kuanzia Jumatatu, ataweka dawati maalum la wafanyabiashara watakao bughudhiwa au kuzungushwa zungushwa, waripoti kwake direct, halafu huyo afisa anayewazungusha, ataipata habari yake!.
Kiukweli, watu wa aina ya DC Makonda, ndio wanaohitajika kukabidhiwa ofisi za umma na nafasi za mamlaka kama hili jiji la Darisalama, akikabidhiwa Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Darisalama, kiukweli jiji litanyooka!.
Natoa wito kwa Mhe. Rais Magufuli, kufuatia RC wa DSM, Said Meck Sadick kufikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria, (just by look), tunakuomba ututeulie DC Paul Makonda awe RC wa DSM, atakusaidia sana wewe na serikali yako, katika utekelezaji wa falsafa yako ya "HAPA KAZI TUU!". Huyu jamaa akiwa RC DSM, atakula sambamba na vibaka wote na vijana wanaoshinda vijiweni kwa kuwabunia shughuli za kufanya. And you never know hata ile biashara ya wale dada zetu ile, inaweza kupangiwa utaratibu mzuri wa kueweka na hata kuirasinisha kwa kuihalalisha!.
Katika sherehe hiyo ya Malkia wa Nguvu, DC Makonda amedhihirisha wazi yeye ni Balkia wa Nguvu!.
Hongea Sana DC Makonda, sasa unastahili U RC-DSM!.
Naomba kuwasilisha.
Paskali