Nimemfumania mke wangu, nifanyeje?

Nimemfumania mke wangu, nifanyeje?

Mr Bean

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2018
Posts
206
Reaction score
178
habari wadau,

leo asubuhi saa 3 wakati tukiwa nyumbani mie nlimwambia mke wangu kuwa nitaenda umtembelea rafiki yangu na hivyo nitarudi mchana kuja kula nyumbani.

nlipoenda kwa rafiki yangu nikamkuta hayupo, hivyo ikabidi nirejee nyumbani saa 5 asubuhi.

nlipofika nyumbani nkasema ngoja nimfanyie suprise mke wangu, nikafungua mlango kimya kimya na kuingia ndani.

nikawa na nyata nyata hadi chumbani, ila nikamkuta hayupo chumbani.

nika nyata nyata tena hadi sebuleni, napo pia nikamkuta hayupo.

nika nyata nyata tena hadi chooni, pia nikamkuta hayupo.

nikajua itakua yupo jikoni labda anapika,, nika nyata nyata hadi jikoni ndipo nlipomfumania akiwa anadokoa nyama kwenye mchuzi.

sisi nyumbani huwa tunakula nyama siku za holiday tu, imeniuma sana kwa kweli.
 
Wewe kweli ni Mr bean!
Yaan umeenda kwa rafikiako ukamkuta hayupo (umemkuta alafu hayupoí ½í¸‚í ½í¸í ½í¸€
Basi wewe mchukue tu mkeo muende chumbani ukamlambelambe huo utamu wa nyama mdomoni
 
Polee sana Mkuu,siku nyingine usirudie kumtafuta rafiki yako manually, usingemkosa kwake,na hivyo usingemfumania mkeo akidokoa nyama!
 
Bean cku zote story zake huwa za uongoooooo. Ukianza tu kusoma utajua kamba hizi
 
Mzee wa kunyata nyata. Unaujua ule wimbo NIMETEMBEA KIDOGO KIDOGo nikanyata nyata
 
Back
Top Bottom