Aisee watu waliokulia imani flani ni ngumu kutochangama na mabo hayo. Mimi nimetoka kwenye familia ya kichaga watu bado wana imani za mizimu na huku wanaenda kanisani. Nishaona Tanga watu wanasoma kisomo cha Koran wanaisomea mizimu, kisha wanachinja na kufanya matambiko. Sharti kila kilichopikwa ni marufuku kwenda nacho nyumbani, lazima kiliwe sehemu iliyokuwa inaabudiwa. .
Mdogo wangu akiwa mdogo alipelekwa mwananyamala kwa kuingiza mbegu ya chungwa puani. Madaktari walichoma sindani mishipa yote ili mtoto apige chafya lakini wapi. Alikuwa anapumua kwa shida sana madaktari walipambana sana. Mzee kuona haieleweki akatoka nje ya hospital, akatema mate chini na kuomba mzimu kwa kichaga "vameku na vasheku va kasha, ngivaitereveni.....". Mzee kuingia wodini kumshika mtoto kapiga chafya mbegu kule 🙂
wale madaktari walishangaa sana ila ndo ikawa hivyo.
Ila Mungu anaweza, na vijawa wamtafute kwa kuwa Mungu anafanya miujiza mikubwa zaidi. Roho wa Bwana ametenda makuu mengi zaidi ya haya, nimeona hili kupitia mke wangu. Bwana ni Mwema siku zote, msiache kumsihi. .