Nimemchoka sana mama yangu

Nimemchoka sana mama yangu

lady Jay

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2016
Posts
529
Reaction score
655
Habari zenu wapendwa,

Mimi ni msichana niliyemaliza chuo lakini natafuta kazi. Naishi na wazazi wangu na wadogo zangu wa kike ambao nawapenda sana. Nimekulia na kulelewa na bibi sana na mama mdgo ambao wote walikua wapole na wakarimu ila mama mdogo alitangulia mbele ya haki.

Nilimpenda sana mamdogo kuliko mama yangu mzazi kwasababu alinipenda na kuchukua nafasi ya mzazi wangu na ndiye aliyeniambia mume wake mama siyo baba yangu mzazi ( ila ni baba yao wadogo zangu ) nikiwa darasa la sita.
Niliumia sana kwasababu mama yangu alikuwa hana time kabisa kunieleza hayo. Hapo form one ndo nikaanza kuishi na mama yangu ila jamani ni mkali kwangu adi naliaga. Kuna siku nilimuuliza mama mdgo kama huyu kweli ni mama yangu mzazi au la akasema ndo mamako.

My mum hana ukaribu na mimi, ananifokea kila wakati bila hata sababu. Hanaga shukrani in anything i do. Uzuri darasani nilikua nafanya vzuri sana nikishuka position kidgo atafoka likizo nzima. Nilikua nashika nafasi ya nne nikiwa naongoza wasichana ila nikiwa tu wa tano ataongea likizo nzima.

Anavyokuwa ananiangalia, utafikiri yeye ndo mama yangu wa kambo hata akipiga honi ya gari getini nikiwa tu nje nilikua nakimbilia chooni. Anyway namshukuru kwasababu yeye ndo aliyenisomesha. (japo ni wajibu wake).

Tatizo ni pale mama anavyokuwa hana mother to daughter love au affection. Hajali what I do. Naweza kumuomba hela anakuwa mkali mpaka namwambia basi mama natafuta njia napata na haulizi ila wadogo zangu wanapewa hata extra. Mimi sijawahi kununuliwa simu na mama ila wao wananunuliwa tena mimi ndo namsindikizaga mama kununua na haniulizi mimi napata wapi simu.

Nikitaka tuongee labda angalau nimwambie kitu kinachonisumbua au just kupata faraja ya mama anaongea kwa ukali kwamba kachoka au bwanae ondoka ila roho inaniumaga. Marafiki zangu wanavyoongelea mama zao huwa nawatazama na kuwatamani.

Nyumbani kuna mfanyakazi lakini kazi zote nafanya mimi na mama humtetea dada na kusema mimi sina umuhimu ndani wakati kutwa nzima mimi ndo najishughulisha ila nakaaga kimya hadi nikiwa chuo nikija kusalimia huwa hataki niondoke ili nifanye kazi. Nikimwambia mama nina test atasema bwanae kwani wewe wa kwanza kusoma mpaka nakosa raha nikiwa chuo nakuwaga very lonely na mawazo. Sikufanikiwa kupata mkopo wala hela ya matumizi hvyo nilikua nahudumiwa na mama. Aisee sitokuja kusahau mateso niliyopata chuo.

Nimelala hungry nights mpaka ilibidi nizoee. Hapo ndo nikaona nitakufa nikaanza mahusiano na wanaume kisa nipate hela. Hapo mama uwezo anao wakunisaidia lakini anasema hana hela nitafute wanaume tena kwa ukali.

Anyway nilipunguza ukaribu na mama hata upendo kwasababu nilijaribu kuwa karibu nae nipate mapenzi ya mama lakini nikashindwa. Afu yeye ndo anasema nina roho mbaya, sina upendo kama wadogo zangu. Ninamwangalia tu kwasababu najua yeye ndo hanipendi. Na anasema hivyo kwasababu anawasikiliza sana yuko karibu nao but she pushes me away yaani utafikiri niliokotwa.

Kuna wakati huwa natamani niolewe ila ndoa ina majanga yake pia na sina hata mtu. Na hali ya mama imenifanya nikose upendo kwa watu wengne niponipo tu all alone. Kuna wakati nakaa tu na kulia na kinachoniuma nikiwa 7 yrs nilishawahi kubakwa kijijini kwa bibi na mfanyakazi ila sijawahi kumwambia mama wala mtu yeyote.

Watu watakua wanajiuliza mbona sitaji baba. Baba yangu ana familia yake mkoani na alishasahau kama ana mtoto. Baba yangu wa kambo yupoyupo tu but sana sana anawajali wanae ila hainiumizi roho. Ninachomuomba Mungu niondoke nipate kazi hata mkoani mbali na mama yangu.

NB. Wazazi wa hivi especially wamama jaribu kuweni karibu na watoto wenu kuweni na upendo. Mimi siwezi elezea kila kitu hapa ila umuhimu wa mamangu ni kunisomesha tu tena kwa maneno namshukuru sana kwa hilo.

Wapendwa sjui mtanisaidiaje but nimevumilia sana ni mama yangu huyo ndo maana wengne hukimbia kwao au kutaka ndoa haraka ili waondoke makwao.

Wazazi badilikeni tafadhali.
 
Something wrong,sio bure mama awe ana react hivo kwako tu jaribu kuwauliza ndugu zake na uwaambie hali halisi ilivyo wanaweza kukusaidia kufaham tatizo nnini au pengine yeye anaona yupo sawa kwa kuwa ni mama lakini wewe unaona anakuendea sivyo
 
Pole sana!
Kutakua na story nyuma ya kuzaliwa kwako... Wazazi wengine wanahamishia chuki na hasira kwa watoto.
Tafuta kazi ukipata hama hapo kajitegemee... Ipo siku mama yako atajirudi tu. Jaribu kumpenda hivyohivyo alivyo.
Mungu ndo amekukea kukufikisha hapo! Mtumaini yeye!
 
Pole dada,ndo changamoto za maisha hizo afadhali wewe hata mama yako kakusomesha kama mimi sijawahi onja ile raha ya kuwa na mama na nilipofikisha miaka 7 sijawahi ishi nae tena mpaka leo.......mi naona kinachomsumbua mama yako ni uoga wa kuonekana anakujali wewe zaidi kuliko wadogo zako wa hao baba yako mdogo na anadhani itakuwa ugomvi sababu hata wanaume pia baadhi tuna gubu kama wanawake ukiona mwanao hapendwi sana unakuwa ugomvi hasa kwa mke ambae umemwoa tayari ana mtoto/au wote mmeoana mkiwa na watoto,kingine anaona kama unamzibia nafasi sababu ushakuwa mkubwa na anatamani uondoke ili afurahie kikubwa kwako ni omba upate ajira ili utoke hapo kwake au ukipata fursa yoyote jitahidi uifanye upate pa kuanzia kwa umri ulonao hupaswi kujilizaliza kama bado mtoto,tambua kuwa unaweza fanya kitu pasipo kumtegemea mama yako kila kitu....ukiendelea kulialia unakaribisha vidonda vya tumbo bure huku mama yako akiishi maisha safi
 
Kwa sababu tayar u have been living with this kwa muda mrefu na tayar umeshamjua alivyo bas huna haja ya kuweka chuki endlea kuish kama amabavyo anataka yeye soon utaanza kuish maisha yako na utaondokana na hzo kero.
Ila mbna kama mama mdogo ndio mzaz wako ila wamekuficha tu juu ya hilo
 
Kiukweli inauma sana na kama kunakidonda kinacholeta maumivu moyoni basis ni hiki....kupoteza au kutokupata penzi la wazazi...daima tunaamini mama au Baba ndio wenye mpnz ya dhati... Wao mapnz yao ni kama titi lilojaa utamu ambao huupati kwenye maziwa asali wala choculate au sehemu nyingine yoyote ileee....ni pnz hili linalofanya hata kama umezaliwa kwenye familia maskini kama Mimi uridhie hali ilee au ulale na njaaa utaona kawaida kabisa....kwasababu pnz LA dhati, adhimu na adimu umelikumbatia na kuliishi moyoni mwako!!!... Nakushauri njia pekeee ya kuondonakana na hali ya upweke ni kutafuta marafiki kama sio mitaani basi rudi kwenye dinii yako. Angalau utapata MTU ambaye utashare Naye maumivu haya yootee kwasababu kunaathari kubwa mno ya kuwa na mawazo mfululizo. Kwako na kwa kizazi chako. Kuwa makini sana juu ya hilo sii jambo LA kawaida kabisa. Mungu akusaidie upite salama kwenye bonde hili ngumu na lenye mtihani... Ubarikiwe.
 
Ooh! My God pole sana. Yaani mimi nakuelewa sana unayoyasema, maana hata mimi nilishawahi kupitia hayo kipindi fulani katika maisha. I feel like crying umenikumbusha mengi na mbali sana! Believe in God this too will pass
 
kuna kitu sio bure kbs......ulizia kwa marafik wa mama yako kama mama yako aliwah kubakwa au kifanyiwa na unyama na baba ako
 
Ooh! My God pole sana. Yaani mimi nakuelewa sana unayoyasema, maana hata mimi nilishawahi kupitia hayo kipindi fulani katika maisha. I feel like crying umenikumbusha mengi na mbali sana! Believe in God this too will pass
Amen.Thankyu so much
 
Pole,mitihani hua ya aina nyingi,muombe sana mwenyezi Mungu akupe subra na akuongezee uvumilivu,ipo siku utasahau yote na msamehe ,inshalah utakuja kupata mumeo na utaishi maisha mazuri Inshallah..
 
"Mtumikie Kafiri upate Mradi wako"

Kwakuwa hutaishi naye milele, wewe kaa naye huku ukiwa na malengo yako halafu baada ya muda kidogo utaenda kuanza maisha yako.

Vumilia tu kwa muda kidogo, Wengi wamepitia huko.
 
Back
Top Bottom