Nimemchoka ila nashindwa kumwambia

Huyu binti niko nae kwenye mahusiano ni mwaka sasa na tayari anafahamu nina mke na mtoto. Kila nikimtafutia sababu ili nimuache najikuta nashindwa maana kiukweli hajawahi kunikosea kosa ambalo litanifanya nimuache kiurahisi.

Tangu nimeanza nae mahusiano hakuna hata siku moja ambayo mke wangu amegundua kwamba niko kwenye mahusiano na mwanamke mwingine wa nje. Nahisi namkosea sana mke wangu hivyo nataka niachane na haya mambo ya michepuko nitulie tu na mama watoto wangu.

Nitumie njia gani kumuacha ili asijisikie vibaya ?

Karibuni
Ulimtongoza wa nini, by the way kama ni mzuri nipe namba yake nipite nae alafu ujidai ume mind umuache
 
We bwana alomchoka mtu hawi kama wewe,unampenda sema ndo ivyo Ushakolea,mtoto kakufunga kamba za Kitanga,yani uyo mtoto kama sio mtanga bhas atakua mzaramo maana hao ndo wanaojua kupika watu wakapikika...Braza ushanasa na hunasuki ng'ooooo
 
Mke wako nae ana mchepuko wake km huyu ila wewe hujagundua chochote.
 
HIZO AKILI ZA KUACHA KUCHEPUKA NA MKEO ANGEKUWA NAZO BASI MNGELIKUWA NA FAMILIA BORA SANA.
KAMA MUISLAM FANYA KAMA KUOA WAWILI TU USIJAL
 
Haha watoto wa kike tukisema mume wa mtu sumu mnaona tunawaonea wivu
 
Zungumza naye umweleze dhamira yako mtapatana tu kama mlivyopatana mwanzo shida ni kuwa pengine ulimuahidi kuwa utamuoa bi mdogo anasubili hilo hawezi kukukosea kamwe
 
Unamkaribisha nani sasa?? pambana na uchafu wako..rubbish
Tangu niamke wewe ndo umenifanya nicheke kicheko ambacho nadhani tangu wiki ianze sijacheka.

Nadhani angekua karibu yako ungemnasa na kofi la uso!
 
labda nikuulize tu unafaidi nin hasa huko kwa michepuko tofauti na kwa mkeo?
 
Huyu binti niko nae kwenye mahusiano ni mwaka sasa na tayari anafahamu nina mke na mtoto. Kila nikimtafutia sababu ili nimuache najikuta nashindwa maana kiukweli hajawahi kunikosea kosa ambalo litanifanya nimuache kiurahisi.

Tangu nimeanza nae mahusiano hakuna hata siku moja ambayo mke wangu amegundua kwamba niko kwenye mahusiano na mwanamke mwingine wa nje. Nahisi namkosea sana mke wangu hivyo nataka niachane na haya mambo ya michepuko nitulie tu na mama watoto wangu.

Nitumie njia gani kumuacha ili asijisikie vibaya ?

Karibuni

Ni vigumu sana kuacha tabia yako ambayo umeshaizoea, kama binti unayechepuka naye ni mwaminifu bas endelea naye maana naamini utaacha hapo baada ya hatua chache utaopoa kitu kingine. (Wahenga walisema umeruka majivu umekanyaga moto)

Katika watu wanaongoza kwa ushirikina na madeni bas ni wanawake, wanawake wanaturoga sana wanaume hasa awamu hii ya 5.

Mkuu, kama anaheshimu ndoa yako bs endelea naye haina haja ya kumtafutia sababu utaishia kupigwa password za kiswahili tu na ndoa yako haitakuwa ndoa tena.
 
Back
Top Bottom