Nimemaliza kuongea na Rafiki yangu anayeishi Marekani, Ananiambia 'we are still working from home beacuse of Corona, America is becoming boring place'

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
15,059
2,000
Wewe wengine mpaka leo wamejifungia na wanaangamia ukisema Mungu kaisadia nchi yetu utapungukiwa nini?
Mimi naamini na kumwamini Mungu. Lakini napata ukakasi wa kusema Mungu ndiye aliyetusaidia kwa sababu mataifa karibu yote ya Afrika hayakuathirika sana na korona. Ndiyo maana nimesema jaribu kushughulisha akili zako kidogo uone eg Kenya, Uganda etc vifo ni vichache ku-compare na Ulaya na Amerika. Hata China ukichukuwa population na kulinganisha na vifo bado idadi iko chini. Hivyo unaponiambia Mungu alitusadia sisi mimi nitakubishia kwa sababu kuna nchi nyingine ambazo ziko sawa na sisi au hata vizuri kuliko sisi. Kitu ambacho hujui ni kuwa Tanzania ule mwezi wa 4 na 5 kulitokea vifo vingi tu lakini vilifichwa. Sasa sisi tuliopoteza watu wengi kuliko Uganda na Kenya tikisema Mungu alitusaidia hawa majirani zetu watasemaje? Mungu husadia tu watu wanatimiza wajibu wao. Huwezi kupuuza hatari halafu ukasema eti Mungu atakusadia. BTW mbona hajatusaidia kwenye magonjwa mengine kama malaria ambayo yanaua hata watoto wadogo?
 
lordchimkwese

JF-Expert Member
Nov 16, 2015
1,620
2,000
Hadi dakika hii level seat ishakufa kitamboooo....
Usikute malimao na tangawizi na zile pilipili kichaa ni dawa kweli
 
Mr. Sound

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
616
1,000
Usiseme hivyo,hiyo sayansi yenyewe ni hao hao wanaoteketea ndio wabobezi na maarifa ya sayansi tunakariri kutoka kwao!Sisi na nchi nyingi za Africa kufanikiwa kwenye Corona ni bahati ya mtende!Sio kwasababu tuna Rais mkemia!Hoja nyingine nyepesi nyepesi muwe mnakaa nazo tu vifuani mwenu kulinda heshima zenu!
leo hii mbinu alizotumia magufuli zingetumika na wazungu kisha tukaambiwa ni science hakuna ambae angepinga lakini kwa kua ni mweusi mwenzetu tutapinga mpaka mwisho wa dunia

hata maarifa ya mtu mweusi yanaweza kua sehem ya science hivo tusijidunishe sana kama walivotuaminisha wao kua sisi ni duni
 
Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
4,785
2,000
..Ni bahati ya mtende.

..kwasababu kama ni kumuomba MUNGU, wazungu ndio waliotuletea habari za MUNGU tuliyemuomba.

..sasa imekuaje wao waliotu-introduce kwa MUNGU waathirike kuliko sisi?
Tukisema wewe ni mjinga.
Halafu ukaja na povu uko sahihi maana ndivyo ulivyo
 
Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,095
2,000
leo hii mbinu alizotumia magufuli zingetumika na wazungu kisha tukaambiwa ni science hakuna ambae angepinga lakini kwa kua ni mweusi mwenzetu tutapinga mpaka mwisho wa dunia

hata maarifa ya mtu mweusi yanaweza kua sehem ya science hivo tusijidunishe sana kama walivotuaminisha wao kua sisi ni duni
Hebu tueleze hiyo sayansi iliyotumika!Ugonjwa wenyewe ulikuwa haujajulikana vema namna unavyosambaa!Sasa tuambie ni sayansi ipi iliyofanya kazi hapa Tanzania na ikashindikana huko Brazil!
Ukiniambia Mungu,hapo sio sayansi bali jambo lingine kabisa!
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,896
2,000
Mimi naamini na kumwamini Mungu. Lakini napata ukakasi wa kusema Mungu ndiye aliyetusaidia kwa sababu mataifa karibu yote ya Afrika hayakuathirika sana na korona. Ndiyo maana nimesema jaribu kushughulisha akili zako kidogo uone eg Kenya, Uganda etc vifo ni vichache ku-compare na Ulaya na Amerika. Hata China ukichukuwa population na kulinganisha na vifo bado idadi iko chini. Hivyo unaponiambia Mungu alitusadia sisi mimi nitakubishia kwa sababu kuna nchi nyingine ambazo ziko sawa na sisi au hata vizuri kuliko sisi. Kitu ambacho hujui ni kuwa Tanzania ule mwezi wa 4 na 5 kulitokea vifo vingi tu lakini vilifichwa. Sasa sisi tuliopoteza watu wengi kuliko Uganda na Kenya tikisema Mungu alitusaidia hawa majirani zetu watasemaje? Mungu husadia tu watu wanatimiza wajibu wao. Huwezi kupuuza hatari halafu ukasema eti Mungu atakusadia. BTW mbona hajatusaidia kwenye magonjwa mengine kama malaria ambayo yanaua hata watoto wadogo?
Hivyi unaamini data za China? North Korea? Rwanda? Hehehe
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,408
2,000
Hivi na hizo nchi zingine za afrika ambako corona haikuwasumbua na walikua wakiendelea na maisha yao na hata sasa wanaendelea na maisha yao ni magufuli ndo alikua anaziongoza.Mnaangaika sana kumpaisha magu ata kwamambo ambayo hayaleti sense labda kwa wajinga.
 
Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,153

Hata sasa tukisema turudishe kupimana corona basi utaona wagonjwa wengi wa corona na karibu kila kifo tutaambiwa ni corona. Mimi siamini kuhusu maombi ya corona wala kwamba tumetengeneza kinga ya pamoja dhidi ya corona,hali ilivyo sasa ndio uhalisia wa hicho kinachoitwa corona na hakuna chochote tulichofanya kufanya ndio tuwe na hali hii.
 
Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,153
2,000
Hivi na hizo nchi zingine za afrika ambako corona haikuwasumbua na walikua wakiendelea na maisha yao na hata sasa wanaendelea na maisha yao ni magufuli ndo alikua anaziongoza.Mnaangaika sana kumpaisha magu ata kwamambo ambayo hayaleti sense labda kwa wajinga.
Anachopaishwa Magu ni huo ujasili wa kuamua hivi alivyoamu kwa maana kama angekuwa mwengine pengine basi angefanya kama majirani zetu kwa kuamini ndio njia sahihi ya kupambana na corona.
 
Meshe

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
316
500
Hata mvua zikinyesha utasikia ni juhudu za raisi mwanasayansu!!

Hii inaitwa kuokota embe dodo chini ya mwarobaini!!
 
emmadizzo

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
913
1,000
Ao wazungu ndo wanaotupoteza kwa Mungu
..Ni bahati ya mtende.

..kwasababu kama ni kumuomba MUNGU, wazungu ndio waliotuletea habari za MUNGU tuliyemuomba.

..sasa imekuaje wao waliotu-introduce kwa MUNGU waathirike kuliko sisi?
 
utali

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
707
1,000
Wewe ndio mpumbav,tupe sababu ya kwanini Corona haijaathiri sana nchi za EAC na majirani wa nchi hizo!
Stupid you!Je,approach tuliyoifanya ilikuwa na sababu za kisayansi nyuma yake au ni tulicheza kamari?Kichwa panzi kabisa!
Vipi kama Corona ingekuwa inapiga kama Ebola,tungekuwa wapi leo?

Dah Tigershark umepanic tu!!
Huwezi kucheza kamari kwenye ugonjwa aisee, ni lazima uufahamu ndio uchukue hatua sahihi.
Approach iliyotumika ilitokana na kufahamu sayansi ya “immunology”. Unaweza kuanzisha jambo lakini akatokea mwingine ambaye akalifahamu na kuliboresha zaidi, hivyo usishangae.
Wazungu walitiwa hofu na “wana mipango” wakaingia mkenge wakapuuzia ukweli wa kisayansi na matokeo yake kilichowapata unakijua.
Corona ingekuwa kama Ebola bado nasi tungetumia sayansi hiyohiyo kukabiliana nayo. Ndiyo maana ya kupewa akili na utashi
 
utali

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
707
1,000
Nitakuwa wa mwisho kuamini JPM ana hofu ya Mungu zaidi ya maigizo!Unawezaje kutesa watu halafu unasema una hofu ya Mungu?Kwa Matendo maovu dhidi ya binadamu yanayofanywa na yeye kwa kutumia mamlaka yake,hakuna uwepo wa Mungu ndani yake!

Wewee jamaa wewee hata historia huijui. Kasome habari za wafalme huko tena wale waliobarikiwa zaidi uone kama hawakutesa na kuua maelfu kwa maelfu na bado Mungu aliendelea kuwabariki.
 
utali

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
707
1,000
Hivi na hizo nchi zingine za afrika ambako corona haikuwasumbua na walikua wakiendelea na maisha yao na hata sasa wanaendelea na maisha yao ni magufuli ndo alikua anaziongoza.Mnaangaika sana kumpaisha magu ata kwamambo ambayo hayaleti sense labda kwa wajinga.

Haziongozwi na Magu ila zilichukua ushauri na hatua kama ya Magu, sasaa kwani wewe ukikiri hilo inakusumbua nini??
Huna sababu ya kuonyesha chuki na hasira kwa jambo ambalo hata ukikubali halitokudhuru aisee
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
14,632
2,000
Tuache siasa tuache majungu Magufuli ni mwanasayansi asiekuwa muoga na anaejua nini anafanya. Sio kwamba ana miujiza ila alichoweza kuwaaminisha watanzania ni kwamba corona ni mafua ya kawaida sana kawaida ila haiwezi kushindana na uwezo wetu wa kukabiliana na hali tete au hali ngumu.

Alichofanya Magufuli ni kawaondolea watu hofu na kuiona corona kama mafua ya kawaida that how he won against corona. Hili si swala la kiasiasa ni swala kutambua mambo pia tumshukuru Mungu pia kuwa katupa kiongozi anaweza kuona na kutambua hatari na madhara yake leo tungekuwa na lockdown maisha ya watanzania yangekuaje?

Magufuli he is the hero against corona in the world. Kampeni zinaendelea, wapinzani pamoja na chama tawala wote wanajaza watu kwa maelf kiukweli wakati wa corona tungekuwa na Rais toka CHADEMA mnajua maamuzi yangekuwaje.
Tumshukuru Mungu kwa kutuhurumia,hatukuwa na msaada mwingine ila yeye,Mabeberu walikuwa wametabiri vifo vya maelfu ya watu ktk nchi zetu maskini kwasababu ya hali yetu duni lkn Mungu akawageuzia kibao mambo hayakuwa km walivyotarajia.Narudia tena tumshukuru sana Mungu kwa kutuhurumia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom