Soko lako inategemea na wewe mwenyewe kutoa taarifa zinazojitosheleza biashara ya mtandao inaenda na uthibitisho wa kuliona ni bora ungeyapiga hata na picha ili kuvutia wateja. Pia ukanda wa Mwanza inasemekana huwa mnapenda matikiti yale meusi yenye vidoti ndio hufanya vizuri sokoni na wakati upande wa Morogoro, Dar, Dodoma matikiti yanayopendwa sana sokoni ni ya zebra ilikhali wewe hukueleza hata aina gani. Nakushauri kipindi kingine kuwa mbunifu ili mtu avutiwe na tangazo lako kabla tikiti lipo hukohuko shamba kabla ya kuingia sokoni