nimelia hadi nimechoka ....... hii ni fair jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nimelia hadi nimechoka ....... hii ni fair jamani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Smile, May 2, 2012.

 1. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nipo kijiji nimepata kalikizo masaa kadhaa nimekuja kumuonamgonjwa
  Nimekaa home kidogonikaona nitoke niende kanisani nikafanye maombi kidogo kanisani ni mita kadhaa toka home hapa .
  Barabarani sasa,
  Mara katokea huyu mzee kava tishert yake ya ccm
  Nadhani ndo mtu pekee aliebaki wa ccm hapa kijiji maana navojua kijiji hiki…….
  Nikamsalimia ,shkamoo mzee Fulani…. Ajaitika katoa macho kwa mshangao akaachia na tabasamu kali akaanza
  Smile,smile,smile mwanangu ua la asubuhi leo nitacheka mpaka mwaka kesho yaani jana tu nilimuuliza baba yako uko wapi maana kila siku nakukumbuka mwanangu,ujue siku mama yako anakuzaa mimi ndo nilimpeleka hospt kujifungua.nakwambia ulizaliwa na kilo 4 .5 , mtoto mzuri haijawai kutokea kijiji hiki ..........
  Nilijua utakuwa tu mtoto mjanja kama babu yako ,ujue babuyako alikuwa……….. haitokaa itokee bahati mbaya wewe hukumkuta
  Yaani wewe mtoto sio kama hao wengine wanaenda mjini wanarudi wamevaa yeboyebo kama watotowa mamananihii hapo(akataja mtu)
  Tena kuna Yule mtoto wa balozi nanihii kaka yangu Yule ameniomba nimtafutie mke hapa kijijini yaaningoja nimpigie sasa hivi (akatoa simu-akapiga piga ) ooh naona imezimwa ,badaenitamwambia hili jambo .wewe mtoto lazima tukuchukue …wewe …. Naapa hatukuachi…

  Akaendelea
  Sasa smile… hebu nipe elfu kumi moja hapo nikapate moja motomoja baridi….. nikwamwambia sina
  Basi fanya elfu tano………………………………………………………………………………………………nikamwambiasina
  Basi elfu 2……………………………………………………………………………………………………………..nikamwambiasina
  Hata ka elfu au mia tano tu……………………………………………………………………………………….nikamwambia sina


  Akaniambia wewe mtoto ni mjinga mjinga kama shangazi yako ,na ndo maana nilimuacha akaenda kuolewa na lizee huko…….
  Huko mjini wala huna lolote ,kwanza baba yako ndo anakutumiavihela hela vya kutumia si urudi tu hapa kijijini?
  Huna akili yeyote nilijua tu huna lolote.mjinga mjinga tukama kaka yako ndo maana mke kamkimbia (sina hata bro alokimbiwa na mke jamani)
  Kaolewe tu huko porini… nani anaoa wajinga hapa kijijini …kafie mbali huko… mnajifanya jina kubwa kumbe hamna lolote wapuuzi tu…

  Kaishia zake bado anatukana

  Sijui ni mfanyeje huyu mzee jamani?
  Huu ni uungwana?
  Huu ni utu?
  ngoja nilale kidogo ......
   
 2. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hahahaaaa smile......poleee,binadamu ndivyo tulivyo msamehe bure usijitafutie nuksi bure.
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Smile nashukuru vile umeifanya siku yangu ianze kwa kicheko...

  babu hajatenda haki mwaya.. Msanii tu huyo vile umenyima hela ndio mana kakuponda.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naona umefuzu kozi ya mtambuzi
  Hongera
  OTIS
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  yaani wewe unanicheka my dia.... nimfanyeje?
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  nuksi balaa huyu
   
 7. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kozi ipi nimfanyeje huyu mzee otis
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  We Smile nawe acha kudeka . .sasa hapo cha kukuliza nini?! Ushajua ni maneno ya mkosaji...get over it!!

  Angekua amekutukana toka mwanzo ingekuwaje?!
   
 9. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  uandishi wako Smile
  OTIS
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Sasa Smile na wewe ulikosa hata jero ya kumpa? Ungempa tu akutafutie mume, mwenyewe si unajua ilivyo kazi kumpata mume bora?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nimecheka mpendwa tena haswa lol...

  Achana nae kama ni mtu mzima asiyejiheshimu kiasi hicho...huyo anaonekana ni mbea, mfuatilia mambo ya watu, mzushi, mkosa kazi nk...


  kwani alivosema hayo maneno umetoboka mahali? Umepungua uzito? Potezea kijeshi na nakuhakikishia hutapungukiwa na chochote! Mdharau, mwonyeshe kuwa maneno yake sio lolote wala chochote.

  Kwa kifupi ni maneno ya mkosaji, kama ingetokea umempa hela aliyoomba asingekuponda kabisa!


  Just relax my dear Smile.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ushaamka?
  ahh ungempa mia 5 angekupa sifa za malkia elizabeth
   
 13. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mimi roho yangu nyepesi lizzy...
  ulivopewa ban wewe hujalia?
  pole sana
  karibu tena love
   
 14. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  sikuwa na hata mia dia
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseeee!!!

  Nililie ban kwani nilizaliwa JF?!Ban enyewe hata hainizuii kuingia humu nikitaka.
   
 16. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Pole sana mwaya japo nimecheka mpaka basi lol!
  Huyo mbabu hana lolote njaa tu ndio ilikua inamsumbua,
  Ungemwelewa mapema wala usingepoteza machozi yako kwa mtu alokosa ustarabu km huyo!!
   
 17. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Lol! Msamehe bure Smile..si unajua tena uzee ukikolea hua wanakua na akili kama za watoto?potezea yeye bana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Samehe mamy.....u wont loose anything by letting bygones be so

  Pooole sana maana ni wakati mgumu.....kama hivyo u were going to worship ukapewa na mtihani wa imani juuu...simamia imani yako
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  maneo ya mkosaji hayo
  Ngepata hiyo buku na mia tano ungepewa sifa mpaka basi
  Sasa kakosa alichotaka anaona bora akutukane
  Na aahh (samahani lakini) nilijua ameanza kukutupia nondo uwe mke wake kumbe ni hayo
  Achana nae bana wala asingekuharibia siku
  Ulipaswa udharau na uendelee na mambo yako
   
 20. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #20
  May 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Darling Wifi mzima weye?
  Huyu mbabu hakujua Smile roho yake nyepesi lol!
   
Loading...